ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

PETER MSECHU (TANZANIA) - WINNER TUSKER ALL STARS - 2011

Shindano la Tusker All Stars lililoanza 26 June,2011 limefikia fainali jana tarehe 14 August,2011 kwa washindi watatu kupatikana

Alpha Rwirangira toka Rwanda (TPF 3 - Winner),Peter Msechu toka Tanzania (Mshindi wa 2 – TPF 4) na Davis Ntare toka Uganda (TPF 4 – Winner) wameibuka washindi na wamepata shavu la kupiga show same stage na wasanii wa kimataifa baadaye mwaka huu nchini Kenya....

Washiriki wengine walikua Hemedi Suleiman toka Tanzania,Caroline Nabulime na Amileena Mwenesi toka Kenya,Bernard Ng'ang'a na Patricia Kihoro toka Kenya walishiriki na walikaa wiki 8 na Ma Mc walikua ni Prezentaz maarufu Eve D'Souza toka Kenya na Gaetano Kagwa toka Uganda na mbali na washindi hao 3 kupata shavu la ku-share stage moja na wasanii wa kimataifa,haijafunguliwa kama watapata zawadi au vp....!

Kwa hisani ya Bongostarlink.

Read More......
Monday, August 15, 2011 Posted in | | 0 Comments »

Madee
Ney

Mastaa wa game ya Bongo Flava, Madee a.k.a Hamad Ally na Ney wa Mitego a.k.a Emmanuel Elibarick wameshiriki katika ngoma moja yenye jina la Twende Sawa inayozungumzia baadhi ya matatizo yanayolikabili Taifa letu ukiwemo mgao wa umeme unaoendelea hivi sasa na kuwafanya Watanzania wengi wanaotumia nishati hiyo kujingizia kipato kushindwa kufikia malengo yao huku wengine wakizidi kuyumba kiuchumi na familia zao.

Hiyo ni ngoma yangu mpya 'GEORGE MC' ambayo nimewashirikisha mastaa hao ambao katika hali ya kawaida hawawezi kufanya kazi pamoja kutokana na tofauti zao kimuziki, lakini walikubali kushea nami idea kwasababu ya uchungu walionao kwa Wabongo wenzao wanaoendelea kupiga maktaim wakishindwa kuyafikia maisha bora kutokana na janga la umeme.

Kazi hiyo ambayo imefanyika Bamba Rec, chini ya mtayarishaji, Mubbyzoh tayari imeshadondoka kitaani pamoja na kwenye baadhi ya vituo vya redio ndani na nje ya Dar es Salaam (Pia unaweza kuisikiliza hapo juu kushoto kwenye ShoBiz). Ndugu zangu wasanii, huu siyo wakati wa kufurahishana wakati Watanzania wengi hivi sasa wanapita katika kipindi kigumu cha maisha kwa matatizo kibao yanayoendelea kuikumba nchi yetu, sisi kama kioo cha jamii tunasimama vipi na jamii wakati huu?. Thanx Madee na Ney wa Mitego kwa kukubali kusimama pamoja nami katika kuwafikishia ujumbe wananchi na wahusika wa matatizo hayo.

Kumbukeni kwamba vijana ni taifa la leo siyo la kesho na msiba wa leo huwezi kuwa na uchungu na kulia keshokutwa wakati matanga yameshaanuliwa.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »