ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Fid na Matonya katika pozi

Ishu mpya iliyodondoka ndani ya ebwanadaah hivi punde zinatapakaa kwamba wakali kibao wa muziki wa Bongo Flava wanatarajia kudondoka pande za Iringa kwa ajili ya shughuli moja tu, tamasha kubwa lenye jina la MITIKISIKO.
Mratibu wa ishu hiyo, Edwin a.k.a Eddo wa Redio Ebony FM ya huko aliwataja wakali hao kuwa ni Fid Q, Matonya, Squezeer, Chegge, Madee, Tundaman, Blue, Baby Madaha, Linex, Nay wa Mitego, Dully, Felly na wengine kibao huku wale wapenzi wa mirindimo ya pwani wakirusha vidole juu na kundi la Coast Morden taarabu bila kuisahau bendi kali ya Sweat Noise ya Iringa.
"Pia kutakuwa na mchezo wa masumbwi kati ya mkali Rashid Matumla na 'Snake Boy' na Chupaki wa Iringa. Ishu zote hizo zitagongwa ndani ya Uwanja wa mpira wa Samora, Desemba 6, kuanzia saa sita mchana mpaka saa 12 jioni chini ya udhamni wa Kampuni ya simu za mkononi, Vodacom. Ni zaidi ya burudani," alisema Eddo.

Read More......
Sunday, November 29, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Safu maarufu ya Mpaka Home inayopatikana ndani ya Gazeti la Risasi, J'5, Nov 23, 2009 ilitimiza umri wa miaka minne, sherehe fupi ya Birthday hiyo ilifanyika Ijumaa ya wiki iliyopita katika ofisi zetu zilizopo Sinza, Bamaga, Dar es Salaam. Baadhi ya mastaa wa Bongo waliyowahi kutembelewa na Mpaka Home walikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa katika tafrija hiyo fupi. Hebu cheki tulivyoinjoi.

Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Global Publishers, Richard Manyota aliibariki hafla hiyo kabla ya kuanza rasmi
Nikiwa kama muasisi wa Mpaka Home niliwaeleza wageni waalikwa historia fupi ya safu hiyo
Mkubwa Fella kama mgeni mualikwa alikuwa wa kwanza kutoa maoni yake kuhusiana na Mpaka Home
Akafuata 'Rais' wa Manzese Madee
Kanumba pia alikuwa na machache ya kuongea
Yusuf Mlela naye alisema kitu kuhusu kuiboresha zaidi Mpaka Home
Frola Mvungi wa Bongo Dar es Salaam aliwawakilisha mastaa wa kike katika hafla hiyo
Ray pia alitupa maoni yake mazuri
Kutoka Tip Top Connection, Tundaman naye aliongea
Hatimaye ulifika ule wakati muafaka, siunaona kitu cha keki?
Mimi ndiye nilikuwa wa kwanza kulishwa na Imelda Mtema wa Mpaka Home ambaye kwa pamoja tumeifanya safu hii kuwa juu.
Mimi pia nilifanya hivyo kwake

Akafuata Ray
Yusuf Mlela
Madee
Kanumba
Frola Mvungi
George Kayala (Mhariri msaidizi wa Gazeti la Risasi)
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa ambaye pia alikuwa muendesha shughuli wetu siku hiyo, Amrani Kaima naye alikamua keki
Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda na mshauri mkuu wa Mpaka Home, Luqman Maloto naye pia alipata heshima hiyo
Mara ikafika zamu ya msanifu kurasa msaidizi wa Mpaka Home, Walter a.k.a Ota
Mimi pia nilihusika kumlisha keki, mshauri mwingine wa Mpaka Home, Hamida Hassan a.k.a Sista Doi.
Hapa nikimlisha msanifu kurasa chipukizi wa magazeti ya Global, Frank
Ilifika zamu ya dada Glory ambaye ni secretary wetu ofisini
Mfanyakazi mwenzetu, Ally Mbetu naye aliinjoi kwa kitu cha keki
Mara ikafika zamu ya Aloyce ambaye ni mchoraji kwenye magazeti yetu
Kilichofuata baada ya keki zilikuwa ni picha za pozi kwa ajili ya kumbukumbu
Hapa nimetulia na Kanumba katika pozi la kipole zaidi
Hapa nikitabasamu na Ray
Ray, Imelda wa Mpaka Home na Kanumba
Mwisho niliwashukuru wageni kwa kukubali mwaliko wetu na wote waliyofanikisha hafla hiyo kuwa juu. Wapenzi wasomaji wa Mpaka Home miaka hiyo minne kwetu ni kama changamoto ya kufanya mambo makubwa zaidi ili nyinyi mpate kuinjoi na kufahamu maisha halisi ya mastaa wenu wa Kibongo.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Picha zote nikimuonesha Kanumba (katikati) baadhi ya kurasa za gazeti nilizokuwa na designer, kalba hazijaelekea mtamboni.

Staa wa muvi za Kibongo, Steven Kanumba leo mchana aliibuka ofisini kwetu, Global Publishers na kuongea mambo kadhaa huku akijibu baadhi ya maswali tuliyomuuliza. Baadaye aliibukia upande wangu na kucheki jinsi tunavyoandaa magazeti yetu kwenye computer kabla hayajaelekea mtamboni.

Read More......
Friday, November 20, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Jaymah (kushoto) akipozi na baadhi ya washikaji zake anaosoma nao Malysia
...hapa akiwa na mmoja wa wasanii aliowapa shavu kwenye baadhi ya ngoma zake
Brapper (kulia) ndiye mchizi anayegonga ngoma za Jaymah kupitia studio yake, Good Boys

Kutoka pande za Malysia, binti anayeiwakilisha vyema Bongo kupitia game ya muziki wa kizazi kipya, Jessica Shayo a.k.a Jaymah amedondoka TZ na ishu kibao kutoka huko huku mkononi akiwa na ngoma kadhaa.
Akipiga stori na ebwanadaah.blogspot.com leo Jaymah amesema kwamba, akiwa ni mwanafunzi wa mwaka wa pili kunako chuo Legenda cha huko kwa kiasi fulani amefanikiwa kuitangaza Bongo kupitia muziki wake.
"Japokuwa nyimbo nyingi naimba kwa kiingereza na kidogo kiswahili bado watu wengi wanaoishi Malysia wakiwemo waafrika wenzangu wanafahamu kama Tanzania sanaa ya muziki ipo, mpaka sasa nimesharekodi nyimbo nne kupitia studio ya Mtanzania mwenzangu ambaye nasoma naye huko, Brian Wamala a.k.a Brapper ambazo zinachezwa sana katika klabu za kule.
"Nyimbo hizo ni pamoja na Never Ever, Your Body, Want your to know na Bam bam ambazo baadhi yake natarajia kuziachia katika vituo vya redio hapa home kwa kipindi hiki ambacho nipo likizo...... Mengi zaidi kuhusu Jaymah endelea kucheki na blog hii.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kutoka pande za Sinza, DSM mchizi anayepatikana ndani ya umoja wenye jina la Nitoke Vipi Squard, Mbishi Real ameachia ngoma mpya yenye jina la 'Tozi wa Mbagala' iliyogongwa kupitia Say Records.
Akipiga stori na ebwanadaah.blogspot.com, Mbishi alisema kwamba ngoma hiyo tayari ameshaifanyia video chini ya Kampuni ya Jazz Pictures. "Tayari nimeshaiachia na inaendelea kusumbua kupitia vituo kadhaa vya televisheni".

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Jittman akigonga moja ya shoo zake kabla hajapata ajali
Jitta akiwa amelazwa hospitalini baada ya ajali
Jitta siku chache baada ya kutoka hospitali
Jitta alivyo sasa
Jitta akitabasamu alipokuwa akipiga stori na blog hii.

Kutoka pande za Rock City mchizi aliyenusurika kunako ajali mpaya ya pikipiki iliyotokea huko, Jittaman a.k.a Nzagamba leo aliniibukia ofisini kwetu, Sinza Bamaga tukapiga stori mbili tatu, ambapo alisema kwamba amedondoka kutoka Mwanza juzi na hivi sasa amerudi rasmi kwenye game ya muziki baada ya kukaa bench kwa muda tangu alipopata ajali.
"Hivi sasa ni kazi kwa kwenda mbele na kila ngoma nitakayoachia itakuwa juu kwakuwa nimerudi na idea mpya kibao, ukizingatia kwamba kupitia ajali hiyo nimejifunza mambo mengi. Nashukuru Mungu nimepona kwani hakuna aliyetegea mimi kuwa hivi leo, pia nawashukuru wote walikuwa wananipa moyo wakati nipo kitandani, wakiwemo mashabiki wangu. Ebwanadaah! inampa pole za kutosha mchizi na inamkaribisha tena kwenye game.

















Read More......
Tuesday, November 17, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Huwezi amini, lakini ukweli ni kwamba mwana Bongo Flava, Ramadhani Kasembe a.k.a Dullayo Ijumaa ya wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na watu wasiyojulikana kabla ya kudondoka pande za Amana Hospitali na kushonwa nyuzi kumi mkononi.
"Nilikuwa natoka kwenye Klabu moja iliyopo pande za Uwanja wa ndege majira ya saa 10 alfajiri, nikachukua taksi ini-rush home, kabla gari haijaondoka mara washikaji wawili na demu moja wakavamia ndani ya taksi hiyo na kumuamuru dereva awapeleke wanapotaka wao kitu ambacho mimi nilikipinga, baada ya kubishana kwa muda mmoja alishuka akaja upande wangu na kuanza kunipiga na kisu mfululizo, nilikwepa lakini baadae nikaamua kukimamata ndipo alipofanikiwa kunikata mkononi mara mbili," alisema Dullayo alipopiga stori na ebwanadaah!
Mchizi amesema kwamba baada ya kukatwa na kisu ilibidi ashuke kwenye gari hiyo kitendo kilichowapa nafasi watuhumiwa, wakamtishia dereva kwa kisu hicho ikabidi aondoe gari kwa kasi na kutokomea kusikojulikana. Baada ya hapo msanii huyo alitafuta usafiri mwingine mpaka katika Hospitali ya Amana ambapo alishonwa nyuzi kumi na kuruhusiwa kurudi home. "Mpaka sasa kesi ipo katika kituo cha polisi Sitakishari, Ukonga, Dar es Salaam tunaendelea kuwasaka watuhumiwa," alisema.
ebwanadaah! inatoa pole nyingi kwa Dullayo na kumtakia afya njema, kwani yote hayo yatapita na mchizi atarudi na kuendelea kuipandisha juu game ya muziki wa kizazi kipya.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Wakati makundi mawili yaliyoungana kuangusha burudani, TMK Wanaume Family na Tip Top Connection yakiendelea kufanya maajabu katika shoo zake pale yalipodondoka pande za Vavy, Kigamboni mwishoni mwa wiki iliyopita na kufunika mbaya, misiba imeendelea kuchukua nafasi kunako mradi wa muziki wa kizazi kipya.
Mmoja wa wasanii waliyopo katika muungano huo, Amani James Temba a.k.a Mh. Temba katikati ya wiki iliyopita alifiwa na shangazi yake kitu kilichomfanya awe ndani ya wakati mgumu ukizingatia kwamba kifo hicho kilitokea Wilayani Moshi, Kilimanjaro huku yeye akiwa Dar es Salaam anapoishi.
Akipiga stori na safu hii ndani ya ufukwe wa Navy, Kigamboni walipokuwa wakifanya shoo, Temba alisema kwamba, msiba huo ni pigo kwake na kwa ndugu zake wengine kwani Shangazi yake huyo alikuwa na mchango mkubwa ndani ya familia yao. “Yaani hapa nilipo niko safarini, baada ya shoo usiku huu naondoka kuelekea Moshi kwa ajili ya kuwahi mazishi,” alisema Temba.
Msanii huyo alisema kwaba kutokana na ubize aliokuwa nao kunako game yake ya muziki alishindwa kuhudhuria kwenye misimba mingi iliyowahi kutokea kwenye familia yao lakini huu wa sasa hada budi kuhudhuria na kuungana na wanafamilia wengine katika majonzi.
Mbali na Temba, msanii mwinhine wa muziki huo aliyekumbwa na msiba hivi karibuni ni Mandojo abaye alifiwa na baba yake mzazi. Uwazi ShowBiz inawapa pole wasanii hao, yote hayo ni mapenzi yake Mungu, yatapita.

Read More......
Sunday, November 15, 2009 Posted in | | 0 Comments »

Kabla ya shoo Mox wa Wateule aliagiza kwa fujo
Mox, Mimi, Temba na Stiko wa TMK tukishoo lavu
Mimi, Chegge (wa pili kutoka kushoto) tukipozi na wadau wa Muziki wa Bongo Flava
Kassim a.k.a Kitu cha Awena na Madee 'Rais wa Manzese' (kushoto) wakipozi kwa picha
Taim ilipofika Dj wa Tip Top, Kwembe na Mkubwa Fella walisimama kwenye mashine
Kilichofuata ni TMK Wanaume na Tip Top kupagawisha kama hivi
Shangwe za Chama kubwa ziliendelea mpaka kunakucha

Makundi mawili yaliyoungana kwa ajili ya kuangusha burudani, TMK Wanaume family na Tip Top Connection yaliendelea kuongeza idadi ya shoo zilizofanya vyema pale yalipovamia ndani ya Ufukwe wa Nevy Beach, Kigamboni, Dar es Salaam jana Ijumaa na kugonga shoo ya kijanja.
Shoo hiyo ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano mzuri na kituo cha Redio Magic FM kupitia kipindi chake cha Kwetu Flava, iliwashirikisha pia baadhi ya wakali wa Bongo Flava kama Nay wa Mitego, Kimbunga, Mbishi Real, O-Ten na wengine kibao.
"Baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bongo kwa kazi hiyo, sasa tumerudi home (Dar es salaam), kinachofuata ni kazi kwa kwenda mbele," alisema Fella.

Read More......
Saturday, November 14, 2009 Posted in | | 0 Comments »