Kutoka ndani ya mradi wa filamu Bongo, msanii Hemed Suleiman ametangaza kuipiga chini game hiyo ishu ikiwa ni kuchoshwa na bifu zinazomuandama kila kukicha kutoka kwa wasanii wenzake ambazo zimekuwa zikimkosesha usingizi.
Akipiga stori na ebwanadaah leo, mchizi aliweka wazi kwamba tangu alipoanza kujihusisha na sanaa ya filamu akitokea kwenye muziki amekuwa hana raha na sanaa hiyo kwakuwa kila mara amekuwa akitupiwa lawama kuwa yeye ndiyo chanzo cha bifu na wasanii wengine.
"Kwa masikitiko makubwa nimeamua kuachana na sanaa ya uigizaji wa filamu ili niwe huru na kuifanya familia yangu hasa mama awe na amani kwasababu kila mara nimekuwa nikionekana mimi mbaya mbele ya wasanii wenzangu na jamii kwa ujumla, kitu ambacho kimekuwa kikininyima raha.
"Najua mashabiki wangu watasikitika kwa uamuzi huo mgumu lakini sina jinsi, nitabaki kuisapoti game hiyo nikiwa pembeni. Nitawaacha na muvi kadhaa ambazo tayari nimeshacheza lakini hazijatoka, pia kuna filamu ya mwisho ambayo natarajia kuicheza hivi karibuni kabla sijakaa pembeni rasmi kwakuwa tayari nimeshaingia mkataba na waandaaji," alisema Hemed.
One Responses to "HEMED AIPIGA CHINI SANAA YA MUVI"