



Berry Black kutoka Zanzibar pia atakuwepo
Kundi la muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume family Jumamosi ya wiki hii ikiwa ni mkesha wa kuamkia siku ya kupiga kura, Oktoba 31 litaonesha uzalendo kwa kuwavuta vijana na kuwahamasiaha kujitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo kwenye majimbo yao kupitia shoo yenye jina la 'AMKA KIJANA'.
"Wakati maelfu ya vijana watakaohudhuria siku hiyo wakiendelea kuruka kwa ngoma za TMK zikiwemo Mkono mmoja, Fungeni mikanda na Wapinzani pia watakuwa wakipata hamasa ili siku ya kupiga kura, Oktoba 31, mwaka huu wajitokeze kwa wingi. Sisi kama TMK tunaamini vijana wengi wameshakatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wasiyo waaminifu ndiyo maana tunataka tuwaweke karibu na kuwahamasisha," alisema Fella.
Vilevile meneja huyo alisema kwamba siku hiyo hawatokuwa peke yao, watapigwa tafu na wasanii kama AT, Tundaman, Bi Kidude, Omary Omary, H. Mbizo, Berry Black na kundi la muziki wa taarabu la Five Star. Wewe kama kijana ishu hiyo inakuusu, kwanini siku hiyo usijisogeze pande hizo?
Read More......Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, msanii Aboubakari Katwila 'Q Chiller' amesema na ebwanadaa kwamba, katika kuwahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi Oktoba 31, mwaka huu kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa ukweli ameandaa mpango kabambe aliyoupa jina la Usiku wa Chiller utakaoanzia nyumbani kwao Tanga.
Akipiga stori zaidi, msanii huyo ambaye hivi sasa anasikika na kuonekana kideoni kupitia ngoma yake, 7x70 alisema kuwa ishu hiyo itapigwa ndani ya Tanga Beach Resoat ambapo mbali na kuwahamaisha vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura Jumapili ya wiki hii atafanya balaa pale atakapokuwa anatambulisha ngoma kali zitakazokuwa ndani ya albamu yake mpya.
"Unajua nilikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya kutoa 7x70, kwa hiyo mimi kama kijana na msanii wa siku nyingi nimeona siyo mbaya nikirudi kwenye sanaa kwa nguvu mpya kwa kuanzia nyumbani kwetu Tanga ambapo nitakutana na vijana wenzangu na kuhamasishana ili siku hiyo tujitokeze kwa wiki kwa ajili ya kuwachagua viongozi tunowataka," alisema Chiller.
Pia mchiz alitamka kwamba, kwenye msafara huo atakuwa sambamba na vichwa kibao vikiwemo Domokaya, Bob Junior wa Sharobalo na vingine vya ukweli. Kama wewe ni mdau wa burudani kwanini usijivute pande hizo ukashuhudie ujio mpya wa Chiller.
Read More.........hapa tukisikiliza hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mkuu wa mabalozi wa nchi za Ulaya waliyopo nchini
Lile tamasha kubwa la filamu lenye jina la European Film Festival (EFF) limezinduliwa rasmi jana ndani ya Ukumbi wa New World Cinema Mwenge, Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo mashabiki na mastaa kadhaa wa muvi Bongo walijitokeza kushuhudia tukio hilo ikiwemo filamu King Kong ya Ujerumani ambayo ilifungua pazia.
Katika maonesho hayo yatakayoendelea kwa majuma matatu ndani ya ukumbi huo na baadaye kuhamia Arusha kwa wiki moja, filamu za mataifa zaidi ya 15 kutoka Jumuiya ya Ulaya ‘EU’ zitaoneshwa.
Wadau wa sanaa hiyo kutoka nchi za Ulaya wanatarajia kutoa changamoto kwa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini ili waweze kujua njia sahihi za kukukuza muvi za hapa nyumbani.
Kupitia kwa wakali wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘A.Y’ na Ilunga Kharifa ‘Cpwaa’ upo uwezekano mkubwa kwa mwanadada Ms. Triniti mwenye asili ya Trinidadi na Amerika kuipeperusha Bongo mbali zaidi.
Kauli hiyo ilithibishwa na A.Y alipokuwa akigonga ishu mbili tatu na blog hii juzi ambapo alisema kwamba, kolabo aliyofanya na staa huyo wa kimataifa huenda ikazaa matunda kwa wasanii wa Bongo kupata dili nyingi katika nchi za mbali.
“Nimefanya naye ngoma yenye jina la ‘Goog Look’ ambayo video yake tumepiga Uganda, naamini ataipeleka mbali zaidi na kutufanya Wabongo tutambulike kimataifa,” alisema Ambwene ambaye Jumapili wiki hii atawarusha mashabiki wake ndani ya Club Bilicanas.
Msanii mwingine aliyepiga kolabo na Ms. Triniti aliyekuja Bongo hivi karibuni kwa ajili ya shoo kadhaa ni ‘Cpwaa’.
Kutoka ndani ya lebo ya Shalobalo iliyomtoa ‘dogo’ Nassib Abdull ‘Diamond’ kuna ishu mpya imedondoka pande hizi ikichana kwamba, staa mpya wa lebo hiyo, Mohamed Zimbwe Kassim a.k.a Top C ambaye hivi sasa anasimamia miguu miwili ya ngoma yenye jina la ‘Anko’ amemtupia staa wa Bongo muvi, Riyama Ally kunano video (kichupa) ya ngoma hiyo.
Tofauti na mastaa wengine wa Bongo Fleva ambao kwenye video zao huwapa shavu mamisi na werembo, Top C yeye amesema kwamba alichoangalia ni kipaji cha mwanadada Riyama ambacho kilitakiwa zaidi kwenye video yake.
“Warembo wengine pia wamo kwenye video hiyo ambayo inaendelea kufanya vizuri, lakini nilihitaji kipaji cha kweli kutokana na stori yenyewe jinsi ilivyo kitu ambacho Riyama amekioneshea uhalisia. Baada ya kazi hiyo nimeachia ngoma nyijgine yenye jina la Haya iliyopigwa hapo hapo Shalobalo na Prodyuza Bob Junior,” alisema Top C.
Read More......