Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (wa pili kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Clouds Media, Rugemalila Mutahaba leo, Dar esSalaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda wa miaka miwili kwasababu za kimuziki, huku wapatanishi wa 'bifu' hilo, Waziri wa Habari Utamkaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. (Picha na Anna Nkinda- Maelezo)
Mimi na Zuhura pia tutasababisha stejini kama kawa
Aslay atatambulishwa pande hizo kwa mara ya kwanza
Temba a.k.a Tembelee ataliongoza jahazi la TMK Wanaume family
Tembele 'kichwa kinauma'
Stiko 'Kichwa kinauma'
Bi Cheka 'Kichwa kinauma'
Mkubwa Fella na Wanawe wakiwa mazoezini kujiandaa na shoo hiyo
NI SHOO INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA MASHABIKI WA PANDE ZA MBEZI LUIS NA VITONGOJI VYA JIRANI. MPANGO MZIMA NI MACHI 3, MWAKA HUU NDANI YA UKUMBI WA TIME SQUARE.
Bi. Cheka akiandaliwa na Producer Sulesh wa Poteza Rec, kabla hajaanza kurekodi
Kutoka ndani ya Familia ya Mkubwa na Wanawe, Bibi mwenye umri wa miaka 51 sasa yuko tayari kutoka na ngoma yake ya kwanza kupitia tasnia ya muziki wa kizazi kipya. Anaitwa Bi. Cheka Hija ambaye alipiga stori na ebwanadaah na kuweka wazi kwamba, alikuwa anauzimia muziki tangu miaka ya 1970 lakini ndoto zake zimeanza kutimia mwaka huu mwanzoni alipokutana na Mkubwa Fella. "Niko tayari kutambulisha ngoma yangu mpya ambayo nimefanya na Temba, nina uwezo wa kuimba na kuchana, pia huwa siandiki mistari kwenye makaratasi bali huwa natoa kichwani moja kwa moja,"alisema Bi. Cheka.
Kundi la TMK Wanaume Family a.k.a Watoto wa Kiume watashuka pande za Mbezi Luis, Dar es Salaam kwa kazi mbili za nguvu, kuitambulisha ngoma na muvi yao yenye jina ka Kichwa kinauma pamoja na kumuweka mbele ya hadhara dogo anayefanya vizuri sasa na ngoma yenye jina la Nakusemea, anaitwa Aslay Isiaka. Mpango mzima wa burudani hiyo utachukua nafasi Jumamosi ya Machi 3, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa times Square uliyopo pande hizo, huku wakipewa sapo na wasanii wengine kibao nikiwemo mimi George MC na ngoma yangu Narudi Nyumbani, bila kumsahau 'Shostito' wangu, Zuhura a.k.a Limupenzi ambaye anafanya vyema na ngoma yenye jina la Ukubwa jalala. Pia wasanii wapya wanaoibuka pande hizo watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao vya kuimba na mshindi mmoja atakula shavu la kurekodi ndani ya studio za Poteza Records zilizomtoa Dogo Aslay. Kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa ni shilingi 3000 kwa kila mtu. Njoo wewe na yule mpenda burudani. Mbezi sasa mmekumbukwa.
TEMBELEA DUKA LA KIJANJA, MC VIDEO CLASSIC LILILOPO KIBAMBA (NJIAPANDA YA SHULE), DAR ES SALAAM UJIPATIE MOVIE ZA KIBONGO, COLLECTIONS MOVIES, CD ZA MUZIKI WA GOSPEL, BONGO FLAVA, VIFAA VYA SIMU, UREMBO N.K. KARIBU SANA
UNAJUA KUDANSI?
JE, WEWE NI MKALI WA KUPIGA SHOO NA HAUJUI UTAFANYA NINI?. NJOO UJIUNGE NA BADUGU DANCES. CHEKI NA SISI 0715 110 173, 0787 110 173 , 0717-340387. TIMIZA NDOTO ZAKO.