Huwezi amini, lakini ukweli ni kwamba mwana Bongo Flava, Ramadhani Kasembe a.k.a Dullayo Ijumaa ya wiki iliyopita alinusurika kifo baada ya kuchomwa kisu na watu wasiyojulikana kabla ya kudondoka pande za Amana Hospitali na kushonwa nyuzi kumi mkononi.
"Nilikuwa natoka kwenye Klabu moja iliyopo pande za Uwanja wa ndege majira ya saa 10 alfajiri, nikachukua taksi ini-rush home, kabla gari haijaondoka mara washikaji wawili na demu moja wakavamia ndani ya taksi hiyo na kumuamuru dereva awapeleke wanapotaka wao kitu ambacho mimi nilikipinga, baada ya kubishana kwa muda mmoja alishuka akaja upande wangu na kuanza kunipiga na kisu mfululizo, nilikwepa lakini baadae nikaamua kukimamata ndipo alipofanikiwa kunikata mkononi mara mbili," alisema Dullayo alipopiga stori na ebwanadaah!
Mchizi amesema kwamba baada ya kukatwa na kisu ilibidi ashuke kwenye gari hiyo kitendo kilichowapa nafasi watuhumiwa, wakamtishia dereva kwa kisu hicho ikabidi aondoe gari kwa kasi na kutokomea kusikojulikana. Baada ya hapo msanii huyo alitafuta usafiri mwingine mpaka katika Hospitali ya Amana ambapo alishonwa nyuzi kumi na kuruhusiwa kurudi home. "Mpaka sasa kesi ipo katika kituo cha polisi Sitakishari, Ukonga, Dar es Salaam tunaendelea kuwasaka watuhumiwa," alisema.
ebwanadaah! inatoa pole nyingi kwa Dullayo na kumtakia afya njema, kwani yote hayo yatapita na mchizi atarudi na kuendelea kuipandisha juu game ya muziki wa kizazi kipya.
ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Wakati makundi mawili yaliyoungana kuangusha burudani, TMK Wanaume Family na Tip Top Connection yakiendelea kufanya maajabu katika shoo zake pale yalipodondoka pande za Vavy, Kigamboni mwishoni mwa wiki iliyopita na kufunika mbaya, misiba imeendelea kuchukua nafasi kunako mradi wa muziki wa kizazi kipya.
Mmoja wa wasanii waliyopo katika muungano huo, Amani James Temba a.k.a Mh. Temba katikati ya wiki iliyopita alifiwa na shangazi yake kitu kilichomfanya awe ndani ya wakati mgumu ukizingatia kwamba kifo hicho kilitokea Wilayani Moshi, Kilimanjaro huku yeye akiwa Dar es Salaam anapoishi.
Akipiga stori na safu hii ndani ya ufukwe wa Navy, Kigamboni walipokuwa wakifanya shoo, Temba alisema kwamba, msiba huo ni pigo kwake na kwa ndugu zake wengine kwani Shangazi yake huyo alikuwa na mchango mkubwa ndani ya familia yao. “Yaani hapa nilipo niko safarini, baada ya shoo usiku huu naondoka kuelekea Moshi kwa ajili ya kuwahi mazishi,” alisema Temba.
Msanii huyo alisema kwaba kutokana na ubize aliokuwa nao kunako game yake ya muziki alishindwa kuhudhuria kwenye misimba mingi iliyowahi kutokea kwenye familia yao lakini huu wa sasa hada budi kuhudhuria na kuungana na wanafamilia wengine katika majonzi.
Mbali na Temba, msanii mwinhine wa muziki huo aliyekumbwa na msiba hivi karibuni ni Mandojo abaye alifiwa na baba yake mzazi. Uwazi ShowBiz inawapa pole wasanii hao, yote hayo ni mapenzi yake Mungu, yatapita.
Makundi mawili yaliyoungana kwa ajili ya kuangusha burudani, TMK Wanaume family na Tip Top Connection yaliendelea kuongeza idadi ya shoo zilizofanya vyema pale yalipovamia ndani ya Ufukwe wa Nevy Beach, Kigamboni, Dar es Salaam jana Ijumaa na kugonga shoo ya kijanja.
Shoo hiyo ambayo iliandaliwa kwa ushirikiano mzuri na kituo cha Redio Magic FM kupitia kipindi chake cha Kwetu Flava, iliwashirikisha pia baadhi ya wakali wa Bongo Flava kama Nay wa Mitego, Kimbunga, Mbishi Real, O-Ten na wengine kibao.
"Baada ya kuzunguka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bongo kwa kazi hiyo, sasa tumerudi home (Dar es salaam), kinachofuata ni kazi kwa kwenda mbele," alisema Fella. Read More......
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa kila Mbongo aliyejitokeza kumpokea dada yetu Eliza aliyetuwakilisha vyema kwenye mjengo wa BBA Revolution japo ametolewa kabla ya kuufikia ubingwa. Hapa mwana blog mwenzangu, mfanyakazi mwenzangu na Mwandishi wa Stori za Big Brother kunako magazeti ya Kampuni ya Gklobal Publishers Hamida Hassani a.k.a Sista Doi au 'B' akipozi na Eliza muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Mwali Julius Nyerere Juzi J'5. Ishu zaidi tembelea ndani ya blog yake, www.sisterdoi.blogspot.com.
Mabibi na Mabwana kupitia hapa ebwanadaah nachukua fulsa hii kumtambulisha rasmi kwenu kijana kutoka pande za Tanga a.k.a TA, aliyeingia kunako mapambano dhini ya Ufisadi kupitia ngoma zake, Tanzania na Mr. President iliyoanza kusikika wiki mbili zilizopita.Akiwa anagonga kazi zake kupitia lebo ya Tongwa Records, mchizi anakwenda kwa jina la R.O.M.A ambayo ni a.k.a jina ambalo limetokana na herufi za mwanzo za ndugu zake wanne waliyomtangulia kuzaliwa katika familia yao. Akiwa anapiga buku ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam hivi sasa mchizi anasema kwamba hali duni waliyonayo Wabongo wengi inampa changamoto ya kuandika na kuzishusha hisia zake kupitia mashairi.
"Ngoma zangu zinalenga kuwatetea watu wa chini hasa waishio mikoani ambao wengi wao huishi kwa mlo mmoja kwa siku wakati wapo vigogo ambao wanamiliki mali nyingi kupitia migongo ya jamii hiyo isiyokuwa na uwezo. Kabla sijachia Mr. President hewani niliandika maneno makali sana kwa uchungu niliokuwa nao, lakini baada ya baadhi ya wadau kuisikiliza kazi hiyo walinishauri nipunguze jazba kwa kuondoka maneno makali mpaka ngoma ikawa fresh na kwenda redioni," alisema R.O.M.A.
Ebwanadaah inampa big up za kutosha mchizi kwakuwa ni miongoni mwa wasanii wachache wanaofanya Hip Hop ya ukweli. Mengi zaidi kuhusu R.O.M.A endelea kuchungulia blog hii yenye ishu za ukweli. Read More......
Kwa upande wake Madee alisema kwamba, yeye hana taarifa na uvumi huo na kwamba alichokiimba kwenye wimbo wake wa Pesa ndiyo ukweli na hana mpango wa kurudiana na Pendo kwakuwa tayari ameshasahau yote yaliyopita na kuganga yajayo.
“Wewe MC George ni kama ndugu yangu, sioni sababu ya kukuficha kuhusu hilo, Pendo mimi siko naye na nilichokiimba ndiyo ukweli wenyewe, kama kuna chombo cha habari kimeandika kuhusu hilo inawezekana wameongea na yeye lakini kwa upande wangu najua tumeshaachana siku nyingi,” alisema Madee.
Akiuzungumzia wimbo mmoja wa Bongo Flava ambao jina na wasanii walioimba hawajafahamika bado unaopinga kuwepo kwa Rais wa Manzese, Madee alisema na ebwanadaah kwamba yeye atabaki kuwa rais wa pande hizo tena wa milele kwani ndiye msanii anayetambulisha vyema maeneo hayo na hata kama watatokea wachache wanaompinga wengi watamsapoti.
“Kama wao wamegoma kunipa kura, kaka zao, dada zao na ndugu zao wengine wamenipa kura na ndiyo maana karibu mikoa yote ninayoenda kufanya shoo wananitambua kama ‘Rais’ wa Manzese, siwezi kushangaa kwakuwa rais lazima awe na wapinzani,” alisema Madee. Read More......
Wakiwa njiani kuelekea Kanda ya Ziwa walishuka katika kijiji kimoja na kushoo lavu na madenti wa pande hizo.
Walipofika pande za Shinyanga, mkuu wa wilaya hiyo (katikati) aliwaibukia sehemu waliyofikia na kuwapa hi, ikiwa ni pamoja na kuwaasa kuhusiana na gonjwa hatari la UkimwiMakundi mawili yaliyoungana pamoja na kupiga kazi kunako mradi wa muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume Family na Tip top Connection mwishoni mwa wiki iliyopita walifunga ukurasa baada ya kumaliza kazi ya kuzunguka katika Mikoa mbalimbali nchini na kuangusha burudani za ukweli.
Akipiga stori na ebwana daah! kwa njia ya simu meneja wa kundi la TMK, Said Hassan Fella alisema kwamba baada ya ziara ndefu iliyoanzia pande za Tabora, Kahama, Geita, Mwanza mjini, Sengerema, Chato na Kakola hatimaye wamemaliza kazi kwa shoo ya ukweli iliyofanyika mjini Bukoba ndani ya Uwanja wa Kaitaba na baadaye Linas Klabu.
"Tunawashukuru wote waliyotusapoti mpaka kufanikisha zoezi hilo bila kuwasahau mashabiki wetu, tunarudi Dar kujipanga kwa ajili ya kuendelea na ishu nyingine," alisema Fella.
Read More......
KARIBU SANA
JE, WEWE NI MJANJA?
UNAJUA KUDANSI?
SHOUT OUT !!
Followers
My Blog List
-
-
-
-
SIMBA SC. YAWEKA SOKONI MAJI YAKE!10 years ago
-
-
HARD PRICE COMING SOON12 years ago
-
-
-
Aslay Akifanya Vitu vyake15 years ago
-
-
-
-














