ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Kiba akiwekwa fresh salon kabla ya kuanza kazi
2Face, Kiba na JK
2Face, Ali Kiba wakijiandaa kuingiza voko
Hapa wote wako tayari
Kazi ikaanza

'Ze vokolisti' waukweli kutoka Bongo, Ali Kiba tayari yupo kwa Obama akikamilisha mpango mzima wa kurekodi akishirikiana na baadhi ya mastaa wa muziki kutoka Afrika.
Ishu kutoka pande hizo zilizodondoka ndani ya ebwanadaah jana zinasema kwamba, tayari Kiba na wasanii kama 2Face wa Nigeria, Fally Ipupa (Congo) Amani (Kenya) na wengine weameshaingiza voko kunako studio moja iliyopo Chicago na siku chache zijazo mzigo utakuwa tayari.

Read More......
Friday, October 29, 2010 Posted in | | 0 Comments »



Game ya muziki wa reggae duniani inazidi kupata pengo baada ya staa mwingine wa staili hiyo, Gregory Isaacs kufariki dunia jana huko London, Uingereza kutokana na maradhi ya Kansa ya ini yaliyokuwa yakimsumbua.
Staa huyo wa reggae ambaye alijulikana zaidi kupitia ngoma yake, 'Night Nurse' iliyotoka 1982, katika maisha yake kimuziki alifanikiwa kutoa albamu zaidi ya 50 ikiwemo ile ya mwisho iliyotoka 2008 ikiwa na jina la 'Brand New Mimi'.
Gregory ameacha mjane na watoto kadhaa. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.

Read More......
Tuesday, October 26, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mandojo katika pozi
Mandojo (kushoto) na Domokaya

Ni masikitiko kwa wana-sanaa hasa wa Bongo Flava. Ipo stori inayovuma kwamba mchizi aliyepandisha wazimu kwa ngoma ‘Nikupe Nini’ a.k.a ‘Kanikamulie maji ya ndimu nina kiu koma’, Joseph Michael ‘Mandojo’ yupo nyuma ya nondo Singida.
Impecable sources wame-shair nasi habari kwamba msanii huyo amefungwa miaka miwili jela lakini haijabainika ni kisa gani ambacho kimempeleka ubayani.
Mshirika wa Mandojo, Precioust Juma ‘Domokaya’ last saturday aliimegea blog hii kwamba hata yeye ishu hiyo bado hajaipata fresh, anachojua ni kwamba mchizi yuko nyumbani kwao Manyoni, Singida kwa ajili ya matatizo ya kifamilia likiwemo lile la kufiwa na baba yake mzazi. “Mi pia sijui chochote kuhusu hilo kwa sababu sijapata simu au taarifa yoyote kutoka huko, siwezi kulizungumzia hilo sana,” alisema Domo.
Tangu wiki iliyopita blog hii imekuwa ikipokea simu na SMS za kumwaga kuhusu habari ya mchizi kwamba hana uhuru wa kawaida kama raia wa Tanzania.
“Mandojo kafungwa miaka miwili jela, hukumu imetolewa muda mfupi uliopita,” one of impecable sources alituma SMS kwa gazeti hili.
Wasanii mbalimbali wakubwa pia walimwaga data kwamba Mandojo ameingia kifungoni kwa kosa la kupigana na washkaji wengine wa pande hizo.
Mandojo akiwa na Domokaya, walitikisa soko la Bongo Flava kati ya mwaka 2003 na 2004, walipotoka na ngoma Nikupe, wakafyatua Dingi, Wanoknok ft Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Taswira ft Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’, na nyinginezo kali.
Kwa vyovyote vile, hii si habari njema kwa wapenzi wa muziki na sanaa yetu kwa jumla, ni vema kumuombea Mungu jamaa avuke salama katika kipindi hiki kigumu.

Read More......
Monday, October 25, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mkono mmoja juu
Temba na Chegge
Bi Kidude ndani

Berry Black kutoka Zanzibar pia atakuwepo

Kundi la muziki wa kizazi kipya, TMK Wanaume family Jumamosi ya wiki hii ikiwa ni mkesha wa kuamkia siku ya kupiga kura, Oktoba 31 litaonesha uzalendo kwa kuwavuta vijana na kuwahamasiaha kujitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo kwenye majimbo yao kupitia shoo yenye jina la 'AMKA KIJANA'.

"Wakati maelfu ya vijana watakaohudhuria siku hiyo wakiendelea kuruka kwa ngoma za TMK zikiwemo Mkono mmoja, Fungeni mikanda na Wapinzani pia watakuwa wakipata hamasa ili siku ya kupiga kura, Oktoba 31, mwaka huu wajitokeze kwa wingi. Sisi kama TMK tunaamini vijana wengi wameshakatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wasiyo waaminifu ndiyo maana tunataka tuwaweke karibu na kuwahamasisha," alisema Fella.

Vilevile meneja huyo alisema kwamba siku hiyo hawatokuwa peke yao, watapigwa tafu na wasanii kama AT, Tundaman, Bi Kidude, Omary Omary, H. Mbizo, Berry Black na kundi la muziki wa taarabu la Five Star. Wewe kama kijana ishu hiyo inakuusu, kwanini siku hiyo usijisogeze pande hizo?

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Banana Zorro na Baba yake wakisababisha stejini
Hawa ni baadhi ya vijana walijivuta pande hizo kusikiliza hamasa
Mzee Zorro akiwakilisha kitamasha zaidi
Chid Benz on stage
K-Sher na MwanaFA walisema na vijana wenzao
Banana Zorro na mshua wake, Mzee Zahir Ally Zorro waliwakilisha vyema
The Big Boss, Ruge (kushoto) na Sebastian Maganga walikuwepo kuwasapoti vijana

Kituo cha redio Clouds FM kiliandaa mpango wa ukweli kwa ajili ya kuwahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura, Oktoba 31, mwaka huu. Katika kutimiza hilo jana lilifanyika bonge la tamasha pale katika viwanja vya Biafra, Kinondoni na hao juu ni baadhi ya wasanii na wadau waliyowakilisha kitamasha.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, msanii Aboubakari Katwila 'Q Chiller' amesema na ebwanadaa kwamba, katika kuwahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi Oktoba 31, mwaka huu kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa ukweli ameandaa mpango kabambe aliyoupa jina la Usiku wa Chiller utakaoanzia nyumbani kwao Tanga.

Akipiga stori zaidi, msanii huyo ambaye hivi sasa anasikika na kuonekana kideoni kupitia ngoma yake, 7x70 alisema kuwa ishu hiyo itapigwa ndani ya Tanga Beach Resoat ambapo mbali na kuwahamaisha vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura Jumapili ya wiki hii atafanya balaa pale atakapokuwa anatambulisha ngoma kali zitakazokuwa ndani ya albamu yake mpya.

"Unajua nilikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya kutoa 7x70, kwa hiyo mimi kama kijana na msanii wa siku nyingi nimeona siyo mbaya nikirudi kwenye sanaa kwa nguvu mpya kwa kuanzia nyumbani kwetu Tanga ambapo nitakutana na vijana wenzangu na kuhamasishana ili siku hiyo tujitokeze kwa wiki kwa ajili ya kuwachagua viongozi tunowataka," alisema Chiller.

Pia mchiz alitamka kwamba, kwenye msafara huo atakuwa sambamba na vichwa kibao vikiwemo Domokaya, Bob Junior wa Sharobalo na vingine vya ukweli. Kama wewe ni mdau wa burudani kwanini usijivute pande hizo ukashuhudie ujio mpya wa Chiller.

Read More......
Sunday, October 24, 2010 Posted in | | 0 Comments »

D-Knob ft Matonya
Quick Rock, D-Knob, Godzilla na Stoper

Kutoka ndani ya studio za 24/7, chini ya Producer Villy zimedondoka ngoma kadhaa ambazo kwa kipindi kifupi zimeanza kuonesha kukubalika kunako jamii ya wapenda burudani.
Ngoma hizo in The Club Anthem ya kwao D-Knob, Godzilla, Stoper na Quick Rock, Flora ya Andre G, Historia ya George MC, Mapenzi ya zamani ya D-Knob na nyingine kibao.
Akisema na blog hii producer Villy ambaye mara nyingi hapendi kujiweka mbele ya vyombo vya habari alitamka kwamba ule muda wa kazi zake kusikika umewadia na kwamba alikuwa kimya akijipanga na kulisoma game. Mengi zaidi kuhusu producey Villy na studio ya 24/7 endelea kucheki na blog hii.

Read More......
Friday, October 22, 2010 Posted in | | 0 Comments »

R. Kelly
Ali Kiba

Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, msanii Ali Kiba anatarajia kuondoka leo kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kugonga ngoma ya pamoja na baadhi ya mastaa wa Afrika, kabla ya kufanya kolabo na staa wa kimataifa, Robert Kelly wa pande hizo.
Kwa mujibu wa msemaji wa ishu hiyo, Christine Mosha ‘Seven’, Ali Kiba ataungana na mastaa wengine kutoka Afrika wakiwemo Navio (Uganda), Amani (Kenya), 2Face (Nigeria), Fally Ipupa (Congo), JK (Zambia), 4x4 (Ghana) na wengine waliopata nafasi hiyo kupitia utafiti uliofanywa na Kituo cha Televisheni cha MTV Base wa kutafuta wasanii wakali kwa nchi za Afrika.
Kabla ya safari hiyo, mwanzoni mwa wiki hii, Kiba anayeendelea kufanya vizuri na video ya wimbo wake wa Hadithi iliyoandaliwa na Mtayarishaji, Malcom akiwa katika mchakato huo wa kusepa kwa Obama alijikuta akidondokea kwenye vikwazo pale aliposhindwa kupata Viza ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Staa huyo wa ngoma ya Usiniseme alifika katika Ubalozi huo uliopo pande za Drive In, Dar Jumatatu asubuhi kwa ajili ya kushughulikia ishu hiyo lakini aliambiwa na mmoja wa maafisa wa ubalozi huo kuwa hawezi kupata Viza kwa sababu pasipoti yake ilikuwa inakaribia kwisha muda na kwamba alitakiwa ‘kuirinyuu’ kitu ambacho alikitekeleza na kufanikiwa kuendelea na safari yake leo. Ebwanadaah inamtakia Kiba kolabo njema na aiwakilishe vyema Bongo huko ughaibuni.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Hatimaye kijana aliyefanya vizuri na ngoma kadhaa miaka michache iliyopita, Ally Mohamed Ahmad a.k.a Z-Anto amefunguka na kupiga stori mbili tatu na ebwanadaah zikiwemo ishu zinazohusu maisha yake ya ndani.
Akisema na blog hii kwa njia ya simu kutoka pande za Kigamboni, msanii huyo ambaye hivi sasa amerudi upya na ngoma yenye jina la Kisima cha malavidavi alitamka kwamba mipango mingi aliyokuwa nayo katika maisha yake ilivurugwa na msichana ambaye yeye humuita mtoto wa kike bila kumtaja jina lake.
“Kwa mfano hivi sasa baada ya kuwa peke yangu nimefanikiwa kufungua saluni huku kwetu Kigamboni iitwayo ‘Kwetu salon’ mipango ambayo nilikuwa nayo kitambo ila mtoto wa kike niliyekuwa naye akanivurugia malengo. Kwa sasa nina kila sababu ya kusema asante Mola kwani jina langu linarudi na biashara zangu zinakwenda kama nilivyotarajia, ‘i am back’,” alisema Z-Anto.

Read More......
Posted in | | 3 Comments »

Cool Boy
Inspector Haroun

Waswahili husema, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Kumbe wakati staa wa Muziki wa Kizazi Kipya, Haruna Kahena ‘Inspector Haroun’ anafanya maajabu na ngoma yenye jina la ‘Mtoto wa geti kali’ nyuma ya pazia alikuwepo mtu aliyefanikisha zoezi hilo.
Namzungumzia msanii Cool Boy ambaye alizaliwa kwa jina la Amily Ally anayesikika hivi sasa na ngoma yenye jina la Ajira. Jamaa alisema na ShowBiz kwamba, kuchelewa kwake kutoka ilikuwa neema kwa wengine kama Inspector ambaye alimuandikia ngoma hiyo ya Mtoto wa geti kali.
“Unajua wengi hawafahamu kama mimi ndiye niliandika ngoma ya Mtoto wa geti kali nikampa Inspector na siku zote huwa naamini hawezi kutoka tena mpaka nimuandikie,” alisema Cool Boy kwa kujiamini. Kauli hiyo ya mchizi tunaitupia hapa na kugeukia upande wa Inspector ambaye wakati tunaelekea mitamboni simu yake haikuweza kupatikana mara moja, tutaendele kumtafuta ili athibitishe hilo.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

A.Y mmoja wa wakali wa muziki wa Bongo Flava wanaofanya muziki 'siriazi'

Bado tupo katika safari ya kuzifanya sanaa zetu za Bongo zipenye mbali zaidi a.k.a kimataifa, tunachotafuta hapa ni mchawi anayetufanya tuendelee kubaki tulipo badala ya kwenda mbali zaidi kama walivyo wenzetu wa nchi nyingine za Afrika. Ndiyo maana tukakuomba wewe msomaji na mdau wa burudani utusaidie kutuambia nini hasa kinasababisha kushuka kwa sanaa zetu.
Leo tunaicheki ishu moja ambayo kwa kiasi kikubwa inaunganishwa na sababu nyingine kibao zinazozifanya sanaa zetu zibaki kuishia hapa hapa nyumbani. Kuna mdau mmoja alinitumia meseji akionesha kusikitishwa kwake na baadhi ya wanasanaa wa Bongo ambao wakipata kujulikana kidogo wanajiweka juu zaidi kuliko jamii inavyowatazama, mimi kama mwanasanaa nikaona siyo mbaya nikiishusha hapa ili wewe msomaji na mpenzi wa burudani tuichangie kwa pamoja.
Kuna mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema kwamba umaarufu una nguvu ya ajabu na unaweza ukambadilisha mtu bila yeye kujijua, kitu ambacho nahisi kama kimeanza kuniingia akilini kwa sababu mimi ni mmoja kati ya watu waliopata bahati ya kuishi na baadhi ya watu ambao kabla hawajajulikana walikuwa tofauti na walivyo sasa. Wapo baadhi yao ambao hivi sasa wamekuwa ni walevi kupita kiasi na kusahau majukumu muhimu yaliyowaingiza kwenye sanaa zao.
Hawaishii kwenye ulevi wa pombe tu, kibaya zaidi hutumia hadi dawa za kulevya ambazo mwisho huwafanya waharibu kazi zao, ikiwemo kuwa na jeuri, kutoa maneno ya kashfa kwa jamii iliyowazunguka na kuwafanya wajulikane na inapotokea wakakosa ushirikiano kidogo kutoka kwa jamii hiyo kutokana na tabia zao hushindwa kuendelea na safari ya sanaa kisha hubaki wakijuta na kumuona kila mtu mbaya, wakati wamejiroga wao wenyewe na mwisho sanaa husika inaonekana haina maana tena.
Mbali na kundi hilo wapo baadhi ya wasanii wetu wanapopata kujulikana kidogo tu, inakua ni tiketi ya kuchukulia mademu au wanaume kwa ajili ya kufanya nao ngono tu na kusahau kwamba sanaa ni moja kati ya ajira muhimu ambayo wanatakiwa waiheshimu. Siku moja niliwahi kushikwa sikio na kuambiwa kwamba, kuna msanii mmoja wa kiume (jina ninalo) kila anapokwenda mikoani kufanya shoo baada ya kazi hulala na wasichana wawili au watatu kwa usiku moja, hebu tujiulize hiyo ndiyo maana ya umaarufu?
Kwa mifano hiyo michache inawezekana kabisa wapo baadhi ya wasanii wanaoingia kwenye tasnia hizo wakiwa hawajui wanakwenda kufanya nini au wakiwa na lengo moja tu la kutafuta majina ili wayatumie kufanya uzinzi na uasherati ikiwemo kwa wasanii wa kike kujiuza kwa mapedeshee ambapo mwisho wanawafanya hata wanaopiga kazi ‘siriasi’ waonekane wababaishaji. Ili tuzipeleke sanaa zetu mbele zaidi umefikia wakati sasa wa kuangalia nani ana nia ya dhati kutuinua na yupi anataka kutupeleka shimoni na tunapombaini tumuondoe kundini kwa kutompa ushirikiano.
Naamini mtu yeyote atakayeingia kwenye sanaa akiamini kwamba ndiyo kazi aliyoichagua kama ajira yake ya kudumu hawezi kutembea bega moja chini lingine juu au kutoa maneno ya kashfa mbele za watu pale anaposikika na wimbo mmoja tu redioni bali atakaa chini na kuumiza kichwa zaidi tena akisikia uchungu kwanini na yeye siku moja asipate mwaliko wa kwenda kufanya shoo Marekani kwa kina 50 Cent kama wao wanavyokuja Bongo. Vivyo hivyo kwa upande wa tasnia ya muvi siamini kama mtu huyo anaweza kujiita yeye ni supastaa kwa kushiriki kwenye filamu moja tu, tena akiwa amechezeshwa kama mhusika wa kazi na siyo ‘stelingi’.
Mwisho namaliza kwa kusema kwamba, wasanii wetu wanatakiwa kufahamu kuwa umaarufu siyo tiketi ya kufanya mambo maovu na kujiona wako juu ya jamii ambayo imewakubali kuwa vioo vyao, wanatakiwa wajione wao ni sawa na watu wengine kwa kushiriki kikamilifu kwenye matatizo ya kijamii pale wanapotakiwa kufanya hivyo inawezekana jamii hiyo ikawashauri na kuwapa mawazo mazuri yatakayowafanya wafike mbali zaidi badala ya kujiona wao ndiyo wao wakati hata ukienda kijijini kwetu ‘Nsemulwa’ hawajulikani. Tubadilike.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Mwakilishi wetu katika shindano la BBA All Stars, Mwisho Mwampamba amedondoka Bongo leo majira ya saa moja na dk 45 usiku na kupokelewa na wadau kibao. Wellcome back bro.

Read More......
Wednesday, October 20, 2010 Posted in | | 0 Comments »






Ile tabia ya sisi Wabongo kutowajali Watanzania wenzetu wanaokwenda kutuwakilisha kwenye mashindano mbalimbali nje ya nchi inaendelea kuwa ya kudumu kitu ambacho kinaifanya nchi yetu iendelee kuwa wasindikizaji mbele ya mataifa mengine huku baadhi yetu tukiishia kulaumu na kushusha kashfa za kumwaga kwa mabalozi wetu hao.
Juzi kati mwakilishi wetu ndani ya mjengo wa BBA All Stars pale Afrika Kusini, Mwisho Mwampamba alionesha kuwashangaza wengi kwa kuambulia nafasi ya nne kwenye mashindano hayo kwakua wengi waliamini ule mkwanja yaani dola laki mbili za ubingwa zingekuja Bongo, matokeo yake zikaelekea Nigeria kupitia mshiriki wao, Uti.
Nachotaka kusema hapa ni kwmaba, kweli Mwisho alistahili kuibuka na ushindi kwakuwa ndiye mshiriki aliyetia fola mwanzo mpaka mwisho wa mchezo, lakini wewe na mimi tulitakiwa tumpigie kura ili ashinde kwakuwa kilichokuwa kikiangaliwa zaidi ni kura na siyo maujanja ya mshiriki mjengoni. Kwa kifupi mimi na wewe hatukutaka Mwisho ashinde kwa kutompigia kura badala yake tukaishia kufurahia vituo vyake ikiwemo ile ishu ya kutuletea shemeji pale alipomvisha pete ya uchumba Mery.
Siyo kwa Mwisho tu, hiyo imeshajitokeza hata kwa wasanii wengine wakiwemo washikaji zetu wa muziki wa Bongo Flava ambao wanapotajwa kuwania tuzo nje ya nchi kura zetu hazihusiki kabisa kuwasapoti wakati kiukweli wanakwenda kutuwakilisha Watanzania. Hebu tujiulize kwanini mamilioni ya BBA yamekwenda Nigeria kwa mara ya pili mfululizo, au kwanini tuzo ya mwanamuziki bora kutoka Afrika iliyotolewa Ufaransa hivi karibuni ilikwenda Uganda tena kupitia kwa Mourice Kirya msanii aliyetolewa na A.Y wa Tanzania? Ukweli ni kwamba, linapokuja suala la kitaifa wenzetu wako mbele sana kuhakikisha washiriki wao wanashinda kwa kuwapigia kura.
Hebu tujiulize kwanini tuzo hiyo isingechukuliwa na A.Y aliyekuwa akiwania naye na ndiye aliyemtambulisha msanii huyo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia ngoma ya Binadamu? Hapo hakutakuwa na jibu zaidi ya "Hatukupiga kura". Jamani tuache roho za kwanini, tujitoe kwa ajili ya kusapoti vitu vyetu, hakuta mtu atakayetoka Ulaya au katika nchi nyingine aje atupigie kura ili wawakilishi wetu wafanye vyema kwenye mashindano mbambali bali ni mimi na wewe unayesoma hapa. Tusiishie kulaumu na kuwaponda pale wanaposhindwa, tujiulize kwanini wameshindwa?
Nina mifano mingi na mengi sana ya kuandika kuhusu udhifu wa sapoti yetu kwa Watanzania wenzetu wanaopata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya nje lakini nashindwa kuendelea kwasababu nahisi wengi wetu tumetawaliwa na chuki mioyoni mwetu pamoja na ubinafsi usiyokuwa na ishu, huku tukisahau kwamba mwisho wa siku safari yetu ni moja na huyo usiyependa kumsapoti inawezekana kabisa ndiye atakayekuzika. Hebu tubadilike jamani, vinginevyo tutaendelea kupiga maktaim mpaka tunaingia kaburini.

MC GEORGE
0715 110 173

Read More......
Tuesday, October 19, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Mimi pia nilikuwepo
Pia nilipata muda wa kubadilishana na mawazo na ndugu yangu Kanumba
Zungu Fedha, mimi na Sajuki
Hapa stori zikiendelea

...hapa tukisikiliza hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mkuu wa mabalozi wa nchi za Ulaya waliyopo nchini


Lile tamasha kubwa la filamu lenye jina la European Film Festival (EFF) limezinduliwa rasmi jana ndani ya Ukumbi wa New World Cinema Mwenge, Dar es Salaam.

Katika uzinduzi huo mashabiki na mastaa kadhaa wa muvi Bongo walijitokeza kushuhudia tukio hilo ikiwemo filamu King Kong ya Ujerumani ambayo ilifungua pazia.

Katika maonesho hayo yatakayoendelea kwa majuma matatu ndani ya ukumbi huo na baadaye kuhamia Arusha kwa wiki moja, filamu za mataifa zaidi ya 15 kutoka Jumuiya ya Ulaya ‘EU’ zitaoneshwa.

Wadau wa sanaa hiyo kutoka nchi za Ulaya wanatarajia kutoa changamoto kwa wadau wa tasnia hiyo hapa nchini ili waweze kujua njia sahihi za kukukuza muvi za hapa nyumbani.


Read More......
Friday, October 15, 2010 Posted in | | 0 Comments »

Aunt Ezekiel pia alipitia kunako tasnia ya urembo kabla ya kuibukia kwenye muvi
Irene Uwoya staa wa muvi aliyetokea kunko game ya urembo

Kupitia Fleva ya ShowBiz inayopatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa leo tunadondoka na baadhi ya maoni ya wasomaji na wadau wa burudani Bongo wakichangi mada ya wiki iliyopita ‘Mastaa wetu na thamani ya Big G’. Ishu ya msingi ni kutaka kuona sanaa zetu zinakwenda mbali zaidi badala ya kuendelea kupiga maktaim kila siku tofauti na wenzetu wa nchi nyingine za Afrika ambao wamefanikiwa kuuza kazi zao mbali zaidi. Cheki chini kwa maoni zaidi ya wasomaji.
Helo! Ningependa suala la prodyuza wa filamu kuwachezesha mamiss ambao hawana vipaji zaidi ya kuuza sura liangaliwe kwani wanakwamisha sanaa ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi.
Pia kwanini wasanii wa filamu hawaigizi utamaduni wa Mtanzania au Mwafrika badala yake hukopi uzungu? Angalia mavazi yao, zungumza yao, kuigiza ufahari (majumba ya Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay) na si Manzese, Buguruni au uswazi. Kingine ni filamu za baadhi ya wasanii wanaojiita mastaa ziko ovyo, wajadiliwe na kutajwa waziwazi kwakuwa wanalitia aibu taifa na jamii za Kitanzania nje ya nchi na kuonekana hatuna mila na tamaduni kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa.
Tatizo lingine ni vyombo vya habari kupenda kuwapa hadhi wauza sura eti “Msanii nguli wa filamu au staa kiwango wa filamu” ili hali mwandishi husika anajua fika huyu ni muuza sura. Badilikeni kwakuwa mnachangia kuua sanaa. Ni mimi mdau wa filamu kutoka Tanga.
************************************

Mambo vipi Fleva ya ShowBiz? Ushauri wangu kwa wasanii wetu wa Bongo Fleva, wanapokuwa wamerekodi wimbo, wasiutoe redioni kwanza mpaka wahakikishe wamekamilisha albamu. Kwa sababu wasanii wengi huanza kuachia singo matokeo yake wanapokuja kutoa albamu zile singo zinakuwa zimeshachokwa kwakuwa zinakuwa zimekaa muda mrefu redioni bila msanii husika kukamilisha albamu. Wahakikishe wanapeleka wimbo redioni huku albamu zikiwa tayari. Naitwa J wa DSM.
*************************************

Kuna ulimbukeni ulioota mizizi kwa waandaaji wa sanaa mbalimbali Bongo. Kwa mfano kwenye muziki kuna baadhi ya watu wanawabeba wasanii wasiokuwa na uwezo. Ukija kwenye upande wa filamu umevamiwa na mamiss wengi wasiokuwa na vipaji, tutafika wapi? Hatutaki majina, tunataka vipaji. Mimi Cking Avara wa Yombo Vutuka, DSM.
**************************************

Kwa upande wangu nadhani tatizo ni Ma-Dj, watangazaji wa redio ndiyo wanaua muziki. Mara nyingi wanacheza nyimbo za wasanii wanaowataka wao. Naitwa Paparazi Venance.
***************************************

Tatizo la hawa mastaa wetu wa Bongo Fleva karibu wote wanaimba nyimbo zinazofanana, kila mmoja kasimama kwenye mapenzi, wajaribu kusikiliza nyimbo tofauti. Kwa mfano nyimbo kama za Msondo, Sikinde zina ujumbe muhimu kwa jamii ndiyo maana zinakaa muda mrefu bila kuchuja. Mimi mdau wa burudani.
***************************************

Wakwamishaji wa sanaa ya muziki wa Bongo ni hawa Ma-Dj na watangazaji wa redio ambao wanabagua nyimbo za kucheza. Naitwa Salum Mzenga wa Kariakoo, DSM.
*************************************

Tatizo kubwa lililopo ni kuiga ndiyo maana hatuendi mbali, wasanii wetu wanatakiwa watafute muziki wa asili ya Kitanzania, pia wajitahidi kurekodi kwenye studio zenye ubora kama wenzetu wanavyofanya. Naitwa Shayo wa Tabora.
*************************************

Kwa mtazamo wangu ni kwamba, muziki wa sasa na zamani ni tofauti. Zamani muziki uliotamba sana ulikuwa wa dansi unashirikisha kundi moja lenye wasanii wengi, yaani bendi na studio zilikuwa chache, hivi sasa wasanii ni wengi, kila mtu anafanya kazi peke yake na studio ni nyingi. Pia muziki wa sasa umekuwa kama Big G kwakuwa wasanii hawajiwekei muda wa kutoa ngoma. Wimbo kabla haujachuja wanatoa mwingine unafunika ule wa mwanzo. Mfano ni Chegge na Temba hawazipi ngoma zao nafasi ya kutosha hewani, yaani ni bandika bandua. Tujaribu kufikiria kipindi cha mwaka 1995 kurudi nyuma, kulikuwa na wasanii wangapi, nyimbo ngapi na studio ngapi?
Halafu tuangalie kuanzia 2000 mpaka sasa kuna wasanii wangapi, nyimbo ngapi na studio ngapi? Ni mtazamo wangu tu, Rama Gamba wa Dododma.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »


Kupitia kwa wakali wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yesaya ‘A.Y’ na Ilunga Kharifa ‘Cpwaa’ upo uwezekano mkubwa kwa mwanadada Ms. Triniti mwenye asili ya Trinidadi na Amerika kuipeperusha Bongo mbali zaidi.

Kauli hiyo ilithibishwa na A.Y alipokuwa akigonga ishu mbili tatu na blog hii juzi ambapo alisema kwamba, kolabo aliyofanya na staa huyo wa kimataifa huenda ikazaa matunda kwa wasanii wa Bongo kupata dili nyingi katika nchi za mbali.

“Nimefanya naye ngoma yenye jina la ‘Goog Look’ ambayo video yake tumepiga Uganda, naamini ataipeleka mbali zaidi na kutufanya Wabongo tutambulike kimataifa,” alisema Ambwene ambaye Jumapili wiki hii atawarusha mashabiki wake ndani ya Club Bilicanas.

Msanii mwingine aliyepiga kolabo na Ms. Triniti aliyekuja Bongo hivi karibuni kwa ajili ya shoo kadhaa ni ‘Cpwaa’.


Read More......
Posted in | | 0 Comments »

Kutoka ndani ya lebo ya Shalobalo iliyomtoa ‘dogo’ Nassib Abdull ‘Diamond’ kuna ishu mpya imedondoka pande hizi ikichana kwamba, staa mpya wa lebo hiyo, Mohamed Zimbwe Kassim a.k.a Top C ambaye hivi sasa anasimamia miguu miwili ya ngoma yenye jina la ‘Anko’ amemtupia staa wa Bongo muvi, Riyama Ally kunano video (kichupa) ya ngoma hiyo.

Tofauti na mastaa wengine wa Bongo Fleva ambao kwenye video zao huwapa shavu mamisi na werembo, Top C yeye amesema kwamba alichoangalia ni kipaji cha mwanadada Riyama ambacho kilitakiwa zaidi kwenye video yake.

“Warembo wengine pia wamo kwenye video hiyo ambayo inaendelea kufanya vizuri, lakini nilihitaji kipaji cha kweli kutokana na stori yenyewe jinsi ilivyo kitu ambacho Riyama amekioneshea uhalisia. Baada ya kazi hiyo nimeachia ngoma nyijgine yenye jina la Haya iliyopigwa hapo hapo Shalobalo na Prodyuza Bob Junior,” alisema Top C.

Read More......
Posted in | | 0 Comments »