ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU






Ile tabia ya sisi Wabongo kutowajali Watanzania wenzetu wanaokwenda kutuwakilisha kwenye mashindano mbalimbali nje ya nchi inaendelea kuwa ya kudumu kitu ambacho kinaifanya nchi yetu iendelee kuwa wasindikizaji mbele ya mataifa mengine huku baadhi yetu tukiishia kulaumu na kushusha kashfa za kumwaga kwa mabalozi wetu hao.
Juzi kati mwakilishi wetu ndani ya mjengo wa BBA All Stars pale Afrika Kusini, Mwisho Mwampamba alionesha kuwashangaza wengi kwa kuambulia nafasi ya nne kwenye mashindano hayo kwakua wengi waliamini ule mkwanja yaani dola laki mbili za ubingwa zingekuja Bongo, matokeo yake zikaelekea Nigeria kupitia mshiriki wao, Uti.
Nachotaka kusema hapa ni kwmaba, kweli Mwisho alistahili kuibuka na ushindi kwakuwa ndiye mshiriki aliyetia fola mwanzo mpaka mwisho wa mchezo, lakini wewe na mimi tulitakiwa tumpigie kura ili ashinde kwakuwa kilichokuwa kikiangaliwa zaidi ni kura na siyo maujanja ya mshiriki mjengoni. Kwa kifupi mimi na wewe hatukutaka Mwisho ashinde kwa kutompigia kura badala yake tukaishia kufurahia vituo vyake ikiwemo ile ishu ya kutuletea shemeji pale alipomvisha pete ya uchumba Mery.
Siyo kwa Mwisho tu, hiyo imeshajitokeza hata kwa wasanii wengine wakiwemo washikaji zetu wa muziki wa Bongo Flava ambao wanapotajwa kuwania tuzo nje ya nchi kura zetu hazihusiki kabisa kuwasapoti wakati kiukweli wanakwenda kutuwakilisha Watanzania. Hebu tujiulize kwanini mamilioni ya BBA yamekwenda Nigeria kwa mara ya pili mfululizo, au kwanini tuzo ya mwanamuziki bora kutoka Afrika iliyotolewa Ufaransa hivi karibuni ilikwenda Uganda tena kupitia kwa Mourice Kirya msanii aliyetolewa na A.Y wa Tanzania? Ukweli ni kwamba, linapokuja suala la kitaifa wenzetu wako mbele sana kuhakikisha washiriki wao wanashinda kwa kuwapigia kura.
Hebu tujiulize kwanini tuzo hiyo isingechukuliwa na A.Y aliyekuwa akiwania naye na ndiye aliyemtambulisha msanii huyo katika nchi za Afrika Mashariki kupitia ngoma ya Binadamu? Hapo hakutakuwa na jibu zaidi ya "Hatukupiga kura". Jamani tuache roho za kwanini, tujitoe kwa ajili ya kusapoti vitu vyetu, hakuta mtu atakayetoka Ulaya au katika nchi nyingine aje atupigie kura ili wawakilishi wetu wafanye vyema kwenye mashindano mbambali bali ni mimi na wewe unayesoma hapa. Tusiishie kulaumu na kuwaponda pale wanaposhindwa, tujiulize kwanini wameshindwa?
Nina mifano mingi na mengi sana ya kuandika kuhusu udhifu wa sapoti yetu kwa Watanzania wenzetu wanaopata nafasi ya kushiriki kwenye mashindano ya nje lakini nashindwa kuendelea kwasababu nahisi wengi wetu tumetawaliwa na chuki mioyoni mwetu pamoja na ubinafsi usiyokuwa na ishu, huku tukisahau kwamba mwisho wa siku safari yetu ni moja na huyo usiyependa kumsapoti inawezekana kabisa ndiye atakayekuzika. Hebu tubadilike jamani, vinginevyo tutaendelea kupiga maktaim mpaka tunaingia kaburini.

MC GEORGE
0715 110 173

Tuesday, October 19, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MIMI NA WEWE HATUKUTAKA MWISHO ASHINDE, UNABISHA?"

Write a comment