"Ni wimbo wangu wa pili kuimba peke yangu yaani bila Kumshirikisha mtu mwingine......wa kwanza ulikuwa unaitwa Wivu haukufanya vizuri, niliutoa mwaka jana. Baada ya hapo nikaaamua kuboresha aina ya muziki wangu...Mimi ndiye yule Dogo Ditto niliyeshirikishwa na Afande Selle katika wimbo wa Darubini kali,Usinichukie, Dunia ina Mambo na nyingine nyingi. Pia Dar es Salaam stand up wa Chidi Benz na Muda umefika ya Chiku Ketto.
Phone namba yangu ni +255 713 556 303 Asanteni".
Haya ndiyo mashairi ya ngoma hiyo
Verse 1: Siwezi Kuishi Bila Upendo wako Ulivyoniteka
Naomba Nihifadhi Kwa Mikono Yako Nisije anguka
Nimezunguka Kutwa Nzima Kama wewe sijamuona
Napigwa Vita Chungu Nzima Lakini Bado Napigana
Choras: Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote
Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako
Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2
Verse 2: Sijasahau Usiku Wa Manane ule Ulivyo Nikana
Mbele Ya Nduguzo Na Bwanaako Yule Ukanitukana
Kwa Mapenzi Nilisimama Kama Chizi Nilionekana
Leo Wakusema Hakuna Najua Waamini Nakupenda
Choras: Wapo walotaka Nikuache Nakusema Sitofika Popote
Ndipo Wakanifanya Niongeze Juhudi Nyingi mpaka siku Niwe wako
Sijali Umenitesa Mara ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe wote Pamoja x2
Bridge: Penzi Letu Liende mbele lisifike Mwisho oooooo
Tuwe Wote Milele Tushinde Vikwazo oooooo
Wapooooo Ooo oooo oo Wapooooooooooo
Wapoooooooo Wapooooooooooooooo
Hook: Sijali Umenitesa Mara Ngapi Ama Nimelia Mara Ngapi
Nia Yangu Ni Moja Siku Moja Tuwe Pamoja Haaaaaa x2
Mwandish wa wimbo huu ni Dotto Bernad Bwakeya (Ditto)
Sunday, October 3, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "NGOMA MPYA KUTOKA KWA DITTO"