ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Dudubaya

Philly Kabago


Kutoka pande za Rock City (Mwanza) msanii Godfrey Tumaini a.k.a Dudubaya ambaye ameamua kupiga kambi mkoani humo ameendelea kutokomea ndani zaidi ili kuwafuata mashabiki wake walioko mbali.

Akipiga stori na ebwanadaah kwa njia simu kutoka pande hizo, Dudu alisema kwamba ameamua kupiga kambi mkoani humo kwakuwa ni nyumbani kwao na kuendelea kutokomea kwenye vijiji vya mbali kwa ajili ya burudani kwa watu wake wa huko.

“Kwa mfano Ijumaa hii (leo) mimi na wanangu tutakuwa Ukerewe na kupiga shoo katika Ukumbi wa Kondeni Beach kabla ya kuelekea Misungwi siku inayofuata (kesho). Katika shoo hizo nitakuwa na wasanii kama Phillbet Kabago, Mr. Hill na ‘kru’ nzima ya Michano Time kutoka Passion FM,” alisema Dudu.

Friday, October 1, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "DUDU, KABAGO WAZIDI KUTOKOMEA"

Write a comment