Kutoka ndani ya mradi wa muziki wa kizazi kipya, msanii Aboubakari Katwila 'Q Chiller' amesema na ebwanadaa kwamba, katika kuwahamasisha vijana kujitokeza kwa wingi Oktoba 31, mwaka huu kwa ajili ya kuwachagua viongozi wa ukweli ameandaa mpango kabambe aliyoupa jina la Usiku wa Chiller utakaoanzia nyumbani kwao Tanga.
Akipiga stori zaidi, msanii huyo ambaye hivi sasa anasikika na kuonekana kideoni kupitia ngoma yake, 7x70 alisema kuwa ishu hiyo itapigwa ndani ya Tanga Beach Resoat ambapo mbali na kuwahamaisha vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura Jumapili ya wiki hii atafanya balaa pale atakapokuwa anatambulisha ngoma kali zitakazokuwa ndani ya albamu yake mpya.
"Unajua nilikuwa kimya kwa muda mrefu kabla ya kutoa 7x70, kwa hiyo mimi kama kijana na msanii wa siku nyingi nimeona siyo mbaya nikirudi kwenye sanaa kwa nguvu mpya kwa kuanzia nyumbani kwetu Tanga ambapo nitakutana na vijana wenzangu na kuhamasishana ili siku hiyo tujitokeze kwa wiki kwa ajili ya kuwachagua viongozi tunowataka," alisema Chiller.
Pia mchiz alitamka kwamba, kwenye msafara huo atakuwa sambamba na vichwa kibao vikiwemo Domokaya, Bob Junior wa Sharobalo na vingine vya ukweli. Kama wewe ni mdau wa burudani kwanini usijivute pande hizo ukashuhudie ujio mpya wa Chiller.
One Responses to "Q CHILLER KUFANYA BALAA TANGA"