Msanii anayefanya vyema hivi sasa na ngoma yenye jina la Kisiwa ch malovedave, Z-Anto ameamua kuwa mjasiliamali badala ya kutegemea muziki peke yake ambao ameutaja kuwa ni game ambayo inakuja na kupotea, siyo kitu cha kukiamini moja kwa moja.
Akisema na blog hii kwa njia ya simu kutoka pande za Kigamboni, Z-Anto alitamka kwamba. "Nimefungua salon yangu, inaitwa Kwe2 Salon, ipo Kigamboni karibu na kivukoni, imepakana karibu na kituo cha mafuta. Huduma zote zipo, ni kubwa na ya kisasa zaidi kwani imegawanyika sehemu mbili, upande wa kike na kiume.
"Nimeamua kufungua salon kwa ajili ya kuendeleza life yangu tofauti na sanaa coz siyo kila siku nitafanya shoo," alisema.
Ebwanadaah inatoa big za kumwaga kwa Z-Anto kwa kufikiria njia mbadala ya kujiongea mkwanja. Mimi na wewe mdau na Mtanzania unayesoma stori hii sasa, twenzetuni basi pande hizo tukapendeze na kumuunga mkono mshikaji wetu.
Sunday, October 10, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "Z-ANTO AAMUA KUWA MJASILIAMALI"