ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Baby J katika pozi
Wolper na Baby J wakipiga stori

Kama haujapata bahati ya kuwa karibu na mastaa wawili waliyo katika tasnia tofauti, Jackline Wolper anayefanya Bongo Muvi na Jamila Abdallah ‘Baby J’ aliyeajiriwa na game ya muziki wa kizazi kipya, huwezi kujua kinachoendelea kati yao zaidi ya kudhani ni mashosti wa kawaida tu.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na safu hii kwa muda mrefu, ShowBiz inakua ya kwanza kukufahamisha kwamba, wasanii hao ni ndugu wa damu a.k.a wa kufa na kuzikana japokuwa mmoja anaishi Zanzibar mwigine Dar es Salaam.
Wakipiga stori na blog hii huku wakionesha ‘love’ ya nguvu, wasanii hao kwa nyakati tofauti walisema kwamba, wao ni mtoto wa mjomba na shangazi na siyo undugu wa kukutana kwenye ustaa tu kama ilivyo kwa wengine.
“Mimi ni mtoto wa mjomba, Jack ni mtoto wa shangazi yangu japokuwa sisi tunaishi Zanzibar wao wako hapa Dar na Pwani, watu weaelewe hivyo,” alisema Baby J ambaye hivi sasa anafanya vizuri kupitia ngoma yake, Mpenzi wangu aliyompa shavu Banana Zorro.
Kwa upande wa Wolper hakuwa na cha kuongeza zaidi ya kusisitiza kuwa undugu wao ni wa kwenye shida na raha.

Friday, October 8, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "KUMBE BABY J NA JACK WOLPER NI NDUGU?"

Write a comment