Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family, Said Hassan Fella kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii kadhaa wa muziki wa kizazi kipya wamejiopanga kugonga shoo za mtaani zenye lengo la kuhamisiaha vijana kujitokeza kwa wingi Oktoba 31 mwaka huu kwa ajili ya kupiga kura.
Akipiga stori na blog hii, Fella alisema kwamba kutokanana kuwa bize na majukumu ya kikazi ili kujipatia kipato watu wengi wakiwemo vijana wanahitaji hamasa ya ziada ili wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura.
"Mimi kama kijana nimeamua kulisimamia hili kwakuwa naaamini vijana wenzangu wengi wako bize wakipambana na ugumu wa maisha kitu ambacho kinaweza kuwafanya wasijitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ndiyo maana kwa kushirikiana na wadau wengine wa burudani tukaamua kuandaa tamasha hili lenye jina la KIJANA AMKA UKAPIGE KURA.
"Tutafanya shoo kadhaa mitaani bure tukianzia Wilayani kwetu Temeke katika kata ya Keko na kuendelea sehemu nyingine tutakazozitaja, lengo likiwa ni kuwatia moyo vijana il wajitokeze kwa wingi kuwachagua viongozi watakaowaletea maendeleo badala ya kusubiri wachaguliwe na watu wengine kama ilivyokuwea miaka iliyopita" alisem Fella.
Monday, October 4, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "FELLA NA STREET SHOW YA KIJANA AMKA UKAPIGE KURA OKT. 31"