Mpaka Home ndiyo safu pekee nchini ambayo inadondoka wanapoishi mastaa wa Kibongo na kupiga nao stopri kuhusu maisha yao, kisha inakushushia wewe msomaji ambaye umekuwa ukiifuatilia tangu ilipoanzishwa miaka minne iliyopita wakiwemo wale wanaotuma meseji zao wakiomba kufahamu maisha ya watu maarufu wanaowapenda.
Staa wa muziki wa Bongo Flava, Hussein Rashid Juma a.k.a Hussein Machozi ndiye anachukua nafasi leo baada ya kutiliwa maguu na Mpaka Home mwishoni mwa wiki iliyopita. Mchizi anapiga maisha yake pande za Kijitonyama, Dar akiwa ni mpangaji ndani ya mjengo mmoja uliyopo 'place' hizo ambazo zinakaliwa na mastaa wengi wa Kibongo. Mengi zaidi kuhusu laifu ya Machozi cheki na intavyuu hapo chini.
Maswali 7 kwake
Mpaka Home: Inakuwaje Hussein. Nje ya muziki unapiga dili gani?
Hussein: Ni mjasiliamali wa kawaida.
Mpaka Home: Maisha ya mastaa wengi hasa wa muziki wa kizazi kipya ni ya kupiga mitungi, kubadilisha wanawake na upungufu wa maadili. Kwako hiyo ikoje?
Mpaka Home: Huo ni ulimbukeni na kuiga, vitu ambavyo vitawamaliza kisanii watu wa aina hiyo.
Mpaka Home: Tangu tufike hapa kwako, hatujaona jinsia ya kike. Vipi kuhusu mpenzi au mchumba?
Hussein: Sina.
Mpaka Home: Unaishije na jirani zako?
Hussein: Niko nao sawa, sijawahi kukwaruzana nao hata siku moja.
Mpaka Home: Msimamo wako ukoje kwa masista duu wanaokusumbua kutokana na umaarufu wako?
Hussein: Niko makini sana, huwa nawapa wrong namba a.k.a namba ya gari.
Mpaka Home: Katika maisha yako umeshawahi kuachwa?
Hussein: Nimeshaachwa na mademu watatu, kipindi hicho hawakuwa mastaa kama walivyo sasa (hakuwataja majina).
Mpaka Home: Unaizungumziaje sanaa yako ya muziki?
Hussein: Ni ngumu yataka moyo. Nawapongeza sana mashabiki kwa kusikiliza kazi zangu.
Historia yake kwa ufupi:
Nilizaliwa 1986 wilayani Manyoni, Singida lakini kiasili mimi ni Mmasai wa Longido, Arusha. Nilisoma Shule ya Msingi Pembe iliyopo Singida mjini 1996-2002, baada ya hapo nikajiunga na Sekondari ya Usagala iliyopo Tanga 2003-2006. Nilipomaliza kidato cha nne nikaenda Mwanza ambako ndiko kipaji changu cha muziki kilipoonekana. Naupenda mkoa huo na wazazi wangu wako huko.
One Responses to "MPAKA HOME KWA HUSSEIN MACHOZI"