ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Abdallah Ramadhani enzi ya uhai wake

Mtangazaji mwandamizi wa kituo cha luninga cha Channel Ten na Radio Magic FM ya Dar es Salaam, Abdallah Ramadhani amefariki dunia juzi baada ya kupata ajali mbaya ya gari huko Mozambique alipokuwa akirejea nchini akitokea Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Abdallah alipokuwa njiani akirejea Dar es Salaam gari alilokuwa akiendesha aina ya Pajero lilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa kabla marehemu ahajakimbizwa hospitali na kufariki siku mbili baadae kutokana na majeraha aliyoyapata kichwani. Mipango ya mazishi inaendelea nyumbani kwa marehemu Ilala, Dar es Salaam.
Blog hii inatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwemo wafanyakazi wenzake na wadau wote wa habari ambao hivi sasa wapo katika kipindi kigumu cha maombolezo. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Sunday, October 10, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MTANGAZAJI CHANNEL TEN, MAGIC FM AFARIKI DUNIA"

Write a comment