Shaa & Fid Q wasanii wenye Swaga za ukweli
Meseji ni zilezile, kukopi na kupesti
Wakati Mwenyezi Mungu kupitia vitabu vyake anaagiza kuwa asiye fanya kazi na asile, binaadamu nao kwa upande wao wamelitii hili na kuingiza yao wakisema kwamba, baada ya kazi faraja. Wengi watajiuliza kwanini tumetoa mfano huu, ili kufahamu nini namaanisha shuka chini.
Unaweza kuuchukulia tofauti usemi huo lakini maana kubwa inayousimamisha ni kuwa baada ya majukumu ya kutwa nzima binadamu wengi hukutana sehemu mbalimbali za burudani ili angalau kupunguza uchovu na hata kupoteza mawazo.
Tunapoizungumzia burudani ni pamoja na muziki, filamu pamoja na nyingine ambazo zina wapenzi wengi ama watu hupenda kuburudika nazo baada ya kazi.
Sisi kama wadau wa burudani nambari ‘wani’ leo tunaitazama sanaa ya muziki hasa wa kizazi kipya ambao uko juu na unaendelea kupaa hewani huku ukiwatoa vijana wengi kwenye umasikini na kuwapatia ajira inayowasaidia kusukuma gurudumu la maisha na familia zao kwa ujumla.
Na unapoizungumzia game hiyo huwezi kukwepa kutaja jina hata moja la mshiriki wa sanaa hiyo, nazungumzia wasanii wake kama Fareed Kubanda a.k.a Fid Q, Sara Kais Shaa, Hamad Ally ‘Madee’ na wengine kibao ambao bado wanakomaa katika fani. Lakini je umewahi kujiuliza ni kwanini muziki huo bado unaendelea kuwa juu? Inawezekana kabisa si kwa sababu nyimbo za sasa zina ujumbe mzito au unaoelimisha zaidi lakini ukweli ni kwamba kazi nyingi katika muziki wa kizazi kipya zinabebwa na swaga (staili) tu za wasanii wa sasa.
Hakuna jipya katika nyimbo zao kwa maana ya ‘meseji’ wanazoimba leo zilishaimbwa toka miaka hiyo wanachokifanya ni kama ‘kukopi na kupesti’ tu lakini ni yale yale yaliyokuwa yakiimbwa na akina Marijani Rajabu.
Hili liko wazi kwani hakuna asiyejua nyimbo za kuwasifia wanawake ama kulilia mapenzi zilizokuwa zinaimbwa na Hayati Hemed Maneti, na ni kipya gani alichokiimba Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye nyimbo zake za sasa .
Mwisho wa yote tunakuja kugundua kuwa utamu wa muziki wa leo unalindwa na Swaga tu za wasanii lakini bado hawajaimba kitu kipya. Kwa kusema hayo tusieleweke kuwa tunawapuuza, ni mtazamo tu .
One Responses to "GAME YA BONGO SASA NI SWAGA TU"