Tofauti na ilivyo kwa wasanii wenzetu hasa wa muziki kule kwa Obama (Marekani) ambao asilimia kubwa hutoka katika familia duni kabla ya kufanikiwa na kuwa matajiri wakubwa, siyo kwetu Bongo msanii kama huna uwezo kipesa utaishia kuzisikia kazi za wenzako redioni au kuzion kwenye luninga.
Hayo ni maneno ya msanii Amily Ally a.k.a Cool Boy ambaye aliwahi kufanya game ya muziki wa kizazi kipya miaka kadhaa iliyopita na kupotea ghafla kabla ya kurudi tena hivi karibuni na kutamka kwamba, umasikini ndiyo ulimfanya aingie mitini na kukiweka kipaji chake kando ili ajiopande upya.
"Kiukweli nilishindwa kuendelea kwakuwa vituo vingi vya redio nilikokuwa napeleka ngoma zangu wahusika walikuwa wanataka mkwanja nduiyo wafanye kazi, kitu ambacho kilinifanya niingie kitaani kusaka ajira itakayoniwezesha kumudu gharama za muziki. Japo sijafanikiwa kivile nimerudi tena kwenye game nikiwa na ngoma yenye jina la Ajira iliyofanyika chini ya mtayarishaji Steve White, ambayo nimeiahia wiki mbili zilizopita," alisema mchizi ambaye aliingia kwenye game kunako 2000 kabla ya kusanda na kurudi tena.
Monday, October 4, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "COOL BOY AWATETEA WASANII MASIKINI"