ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Siku kadhaa baada ya gazeti la Ijumaa Wikienda kupitia safu yake ya Abby Cool & MC George Over the weekend kuripoti ishu ya prodyuza kiwango na Mkurugenzi wa Bongo Records, Paul Matthysse ‘P.Funk Majani’ kumchapa kibao na kumtishia kwa bastola msanii Selemani Msindi a.k.a Afande Sele, ShowBiz imetupiwa stori nyingine mpya kutoka kwa mtayarishaji huyo.

Akifunguka mbele ya blog hii ndani ya studio zake zilizopo pande za Mwenge Bamaga, Dar es Salaam, Majani alisema kwamba alilazimika kurusha kofi moja kwa Afande ili kumtuliza baada ya kuona hawaelewani Kiswahili na kukanusha ishu ya kumtolea bastola.

“Kweli nilimpiga Afande kofi moja tu, baada ya kuona hatuelewani. Mimi nilikuwa namuelewesha kwamba humu ndani nimeweka sheria mpya ya kutovuta sigara kubwa na yeye anafahamu hilo, kwanini alivunja sheria, badala ya kunijibu vizuri akawa anawaka huku akinifosi nimalizie kazi yake wakati kuna pesa nilikuwa bado namdai, pia kwa muda huo nilikuwa nimetoka usingizini, kwakuwa usiku mzima wa jana yake sikulala nikimalizia kazi za watu.

“Kuhusu ishu ya bastola hakuna kitu kama hicho, sikumtishia wala similiki hiyo silaha. Kama niliweza kumpiga kofi moja akatulia kwanini nimtishie bastola? Silaha kama hiyo wanatishiwa watu wenye miili mikubwa au majambazi, siyo Afande Sele,” alisema Majani.

Kupitia Gazeti la Ijumaa Wikienda, Afande Sele alidai kupigwa kofi na kutishiwa bastola na P.Funk ambapo alikwenda kufungua kesi katika Kituo cha Polisi Kijitonyama na kupewa RB iliyosomeka KJN/BR/6950/2010 Shambulio la mwili.

ebwanadaah inawapongeza mastaa hao kwa kuimaliza ishu hiyo kiutu uzima na kuendelea kupiga kazi pamoja, wawe mfano kwa wengine kwakuwa bifu hazijengi.

Friday, October 1, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "MAJANI AFUNGUKA KUHUSU KOFI"

Write a comment