ILI MUZIKI WETU UWEZE KWENDA KIMATAIFA NI LAZIMA TUBADILIKE, SAPOTI YAKO PIA MUHIMU

Sajina katika pozi
Kava ya albamu yake inavyoonekana kwa mbele

Album yenye jina la IVETA ya kwake msanii SAJNA kutoka pande za Rock City inaendelea kukimbiza sokoni ikiwa na ngoma za kijanja zipatazo kumi.
Kwa mujibu wa meneja wa 'dogo' huyo, Kid Bwoy ambaye ametoka hospitalini Bugando, Mwanza hivi karibuni alikokuwa amelazwa, albamu hiyo ambayo iliingia kitaani siku kadhaa zilizopita inaendelea kufanya vyema sokoni na kuleta mapinduzi ya mauzo.
"Albamu hiyo ambayo ilianza kutengenezwa Januari, 2010 na kukamilika Julai, 2010 imewashirikisha wasanii wengine kama Belle 9, Linah wa THT, Josefly kutoka Musoma, Mara pamoja na Pipi. Lengo la kutowapa shavu mastaa wengine zaidi ni kutaka kuonesha uwezo wa Sajna na kuthibitisha kwamba msanii mchanga si lazima atoke kupitia migongo ya wasanii wakubwa," alisema.
Vile vile Kid alisema kwamba, ngoma itakayofuata baada ya Iveta itategemea na maoni ya wadau kwakuwa zote ni kali, japo amezitaja mbili ambazo ni Sitaki Kuumizwa iliyomshirikisha Linah na Roho Mbaya iliyowapa shavu Belle 9 na Pipi zitakazopigiwa kura.
Ngoma nyingine zinazopatikana kunako albamu hiyo ni Binadamu, Mbalamwezi, Udehule, Mganga ft. Josefly, Nadhifa, Subira na Ishara ya Msalaba. Kamata kopi ya Iveta ili usikie dogo alivyoonesha njaa kwa kugonga ngoma zenye ubora mkubwa.

Sunday, October 10, 2010 Posted in | | 0 Comments »

One Responses to "IVETA YAZIDI KUKIMBIZA KITAANI"

Write a comment