Aunt Ezekiel pia alipitia kunako tasnia ya urembo kabla ya kuibukia kwenye muvi
Irene Uwoya staa wa muvi aliyetokea kunko game ya urembo
Kupitia Fleva ya ShowBiz inayopatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa leo tunadondoka na baadhi ya maoni ya wasomaji na wadau wa burudani Bongo wakichangi mada ya wiki iliyopita ‘Mastaa wetu na thamani ya Big G’. Ishu ya msingi ni kutaka kuona sanaa zetu zinakwenda mbali zaidi badala ya kuendelea kupiga maktaim kila siku tofauti na wenzetu wa nchi nyingine za Afrika ambao wamefanikiwa kuuza kazi zao mbali zaidi. Cheki chini kwa maoni zaidi ya wasomaji.
Helo! Ningependa suala la prodyuza wa filamu kuwachezesha mamiss ambao hawana vipaji zaidi ya kuuza sura liangaliwe kwani wanakwamisha sanaa ya filamu kuwa ya kimataifa zaidi.
Pia kwanini wasanii wa filamu hawaigizi utamaduni wa Mtanzania au Mwafrika badala yake hukopi uzungu? Angalia mavazi yao, zungumza yao, kuigiza ufahari (majumba ya Mbezi Beach, Masaki, Oysterbay) na si Manzese, Buguruni au uswazi. Kingine ni filamu za baadhi ya wasanii wanaojiita mastaa ziko ovyo, wajadiliwe na kutajwa waziwazi kwakuwa wanalitia aibu taifa na jamii za Kitanzania nje ya nchi na kuonekana hatuna mila na tamaduni kitu ambacho ni upotoshaji mkubwa.
Tatizo lingine ni vyombo vya habari kupenda kuwapa hadhi wauza sura eti “Msanii nguli wa filamu au staa kiwango wa filamu” ili hali mwandishi husika anajua fika huyu ni muuza sura. Badilikeni kwakuwa mnachangia kuua sanaa. Ni mimi mdau wa filamu kutoka Tanga.
************************************
Mambo vipi Fleva ya ShowBiz? Ushauri wangu kwa wasanii wetu wa Bongo Fleva, wanapokuwa wamerekodi wimbo, wasiutoe redioni kwanza mpaka wahakikishe wamekamilisha albamu. Kwa sababu wasanii wengi huanza kuachia singo matokeo yake wanapokuja kutoa albamu zile singo zinakuwa zimeshachokwa kwakuwa zinakuwa zimekaa muda mrefu redioni bila msanii husika kukamilisha albamu. Wahakikishe wanapeleka wimbo redioni huku albamu zikiwa tayari. Naitwa J wa DSM.
*************************************
Kuna ulimbukeni ulioota mizizi kwa waandaaji wa sanaa mbalimbali Bongo. Kwa mfano kwenye muziki kuna baadhi ya watu wanawabeba wasanii wasiokuwa na uwezo. Ukija kwenye upande wa filamu umevamiwa na mamiss wengi wasiokuwa na vipaji, tutafika wapi? Hatutaki majina, tunataka vipaji. Mimi Cking Avara wa Yombo Vutuka, DSM.
**************************************
Kwa upande wangu nadhani tatizo ni Ma-Dj, watangazaji wa redio ndiyo wanaua muziki. Mara nyingi wanacheza nyimbo za wasanii wanaowataka wao. Naitwa Paparazi Venance.
***************************************
Tatizo la hawa mastaa wetu wa Bongo Fleva karibu wote wanaimba nyimbo zinazofanana, kila mmoja kasimama kwenye mapenzi, wajaribu kusikiliza nyimbo tofauti. Kwa mfano nyimbo kama za Msondo, Sikinde zina ujumbe muhimu kwa jamii ndiyo maana zinakaa muda mrefu bila kuchuja. Mimi mdau wa burudani.
***************************************
Wakwamishaji wa sanaa ya muziki wa Bongo ni hawa Ma-Dj na watangazaji wa redio ambao wanabagua nyimbo za kucheza. Naitwa Salum Mzenga wa Kariakoo, DSM.
*************************************
Tatizo kubwa lililopo ni kuiga ndiyo maana hatuendi mbali, wasanii wetu wanatakiwa watafute muziki wa asili ya Kitanzania, pia wajitahidi kurekodi kwenye studio zenye ubora kama wenzetu wanavyofanya. Naitwa Shayo wa Tabora.
*************************************
Kwa mtazamo wangu ni kwamba, muziki wa sasa na zamani ni tofauti. Zamani muziki uliotamba sana ulikuwa wa dansi unashirikisha kundi moja lenye wasanii wengi, yaani bendi na studio zilikuwa chache, hivi sasa wasanii ni wengi, kila mtu anafanya kazi peke yake na studio ni nyingi. Pia muziki wa sasa umekuwa kama Big G kwakuwa wasanii hawajiwekei muda wa kutoa ngoma. Wimbo kabla haujachuja wanatoa mwingine unafunika ule wa mwanzo. Mfano ni Chegge na Temba hawazipi ngoma zao nafasi ya kutosha hewani, yaani ni bandika bandua. Tujaribu kufikiria kipindi cha mwaka 1995 kurudi nyuma, kulikuwa na wasanii wangapi, nyimbo ngapi na studio ngapi?
Halafu tuangalie kuanzia 2000 mpaka sasa kuna wasanii wangapi, nyimbo ngapi na studio ngapi? Ni mtazamo wangu tu, Rama Gamba wa Dododma.
Friday, October 15, 2010
Posted in | |
0 Comments »
One Responses to "MAMISS WAUZA SURA WASIPEWE NAFASI KWENYE MUVI"