Kila tulipokutana alinipa moyo katika sanaa yangu ya muziki
Nimeamini kizuri hakidumu
Nguzo ya tasnia ya muvi Bongo imeondoka ghafla na kuacha simanzi kwa maelfu ya Watanzania na mashabiki wake walio nje ya nchi. Tangulia Kanumba, kwani hiyo ni safari yetu sote japo hatujui nani ataziba pengo lako. Sisi tuliyobaki tunajukumu kubwa la kuhakikisha tunaendeleza pale ulipoishia. Pole nyingi zitue kwa familia ya marehemu na wote wenye simanzi kama mimi. Tangulia The Great, tuko nyuma yako.
Maswahiba wawili kunako game ya muziki wa kizazi kipa, Selemani Msindi 'Afande Sele' na Hamis Shaban Kinzasa "20% au Twenty Pa' leo wameburuzwa kwa pilato huko mjini Morogoro wakidaiwa kuvamia sehemu na kusababisha vurugu. Kwa mujibu wa mdau mmoja wa ebwanadaah aliyeko pande hizo, Afande na 'shosti' wake huyo walidakwa na polisi jana na kutupwa selo kabla hawajafikishwa mbele ya pilato leo, ambapo kesi hiyo imepigwa kalenda mpaka itakaposomwa tena siku kadhaa zijazo. Zaidi kuhusu ishu hiyo endelea kuchungulia ebwanadaah.
Read More......
Wednesday, April 4, 2012
Posted in | |
0 Comments »
Kutoka ndani ya familia ya Mkubwa na Wanaye, sasa ni zamu ya Bi. Cheka kusimamishwa mbele ya jamii baada ya kazi yake kumtambulisha vyema na kuwafanya baadhi ya mashabiki wasiamini kama na umri wa miaka 51 kuelekea 52. Ishu ni kwamba, Bibi huyu mwenye maskani yake pande za Bagamoyo, Pwani atatambulishwa kwa mara ya kwanza kwa mashabiki wa Morogoro siku ya Sikukuu ya Pasaka ikayoadhimishwa duniani kote Aprili 8, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri. Meneja wake, Said Hassan Fella 'Mkubwa' amesema na Ebwanadaah leo kwamba,Bi. Cheka atapigwa tafu na kundi zima la TMK Wanaume Family, bila kuvisahau vichwa kibao vinavyounda Mkubwa na Wanaye kama Aslay, Dogo Mu, Easy Man na vingine kibao, huku wasanii waalikwa akiwemo Ferooz wakiungurumisha shoo za mwaka 2012. Ebwanaeeeee, Morogoro siku hiyo sogeeni pande za Jamhuri mshuhudia umri mkubwa, damu changa.
Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi (wa pili kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi wa Clouds Media, Rugemalila Mutahaba leo, Dar esSalaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa muda wa miaka miwili kwasababu za kimuziki, huku wapatanishi wa 'bifu' hilo, Waziri wa Habari Utamkaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia. (Picha na Anna Nkinda- Maelezo)
Mimi na Zuhura pia tutasababisha stejini kama kawa
Aslay atatambulishwa pande hizo kwa mara ya kwanza
Temba a.k.a Tembelee ataliongoza jahazi la TMK Wanaume family
Tembele 'kichwa kinauma'
Stiko 'Kichwa kinauma'
Bi Cheka 'Kichwa kinauma'
Mkubwa Fella na Wanawe wakiwa mazoezini kujiandaa na shoo hiyo
NI SHOO INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA MASHABIKI WA PANDE ZA MBEZI LUIS NA VITONGOJI VYA JIRANI. MPANGO MZIMA NI MACHI 3, MWAKA HUU NDANI YA UKUMBI WA TIME SQUARE.
Bi. Cheka akiandaliwa na Producer Sulesh wa Poteza Rec, kabla hajaanza kurekodi
Kutoka ndani ya Familia ya Mkubwa na Wanawe, Bibi mwenye umri wa miaka 51 sasa yuko tayari kutoka na ngoma yake ya kwanza kupitia tasnia ya muziki wa kizazi kipya. Anaitwa Bi. Cheka Hija ambaye alipiga stori na ebwanadaah na kuweka wazi kwamba, alikuwa anauzimia muziki tangu miaka ya 1970 lakini ndoto zake zimeanza kutimia mwaka huu mwanzoni alipokutana na Mkubwa Fella. "Niko tayari kutambulisha ngoma yangu mpya ambayo nimefanya na Temba, nina uwezo wa kuimba na kuchana, pia huwa siandiki mistari kwenye makaratasi bali huwa natoa kichwani moja kwa moja,"alisema Bi. Cheka.
TEMBELEA DUKA LA KIJANJA, MC VIDEO CLASSIC LILILOPO KIBAMBA (NJIAPANDA YA SHULE), DAR ES SALAAM UJIPATIE MOVIE ZA KIBONGO, COLLECTIONS MOVIES, CD ZA MUZIKI WA GOSPEL, BONGO FLAVA, VIFAA VYA SIMU, UREMBO N.K. KARIBU SANA
UNAJUA KUDANSI?
JE, WEWE NI MKALI WA KUPIGA SHOO NA HAUJUI UTAFANYA NINI?. NJOO UJIUNGE NA BADUGU DANCES. CHEKI NA SISI 0715 110 173, 0787 110 173 , 0717-340387. TIMIZA NDOTO ZAKO.